WILAYA ya
Biharamulo Mkoani Kagera ambayo katika matokeo ya ufaulu wa mitihani ya elimu
ya msingi mwaka jana ilikuwa ya kwanza kimkoa na ya pili kitaifa imejipanga
tena kuwa ya kwanza kwa matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka mwaka huu.
Kaimu Afisa
Elimu wilayani Biharamulo Bw. Samweli Sammy amesema hayo jana (April 9) katika
maadhimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika katika shule ya msingi Nyamigogo
iliyokuwa shule ya kwanza wilayani humo kwa matokeo ya mwaka jana.
Kaimu Afisa Elimu
wilaya,
ya Biharamulo,mkoani kagera
Bw.Samwel
Sammy.
|
Bw.Sammy
alisema ufaulu huo utazingatiwa kwa kusimamia taaluma katika shule zote
zipatazo 88 zenye wanafunzi 50711 kati yao wavulana ni 24 966 na
wasichana ni 25 745 wanaofundishwa na walimu 858
waliopo kati ya 1287 wanaohitajika.
Alisema
mikakati iliyopo katika idara hiyo ni kufanya majaribio ya mitihani ya
usuli (Mock) kwa wanafunzi wa darasa la saba na la nne ili kuwafanya
wanafunzi kujenga uzoefu wa kujibu maswali ya mitihani.
“Mafanikio
yatapatikana kwa kutekeleza ugatuaji madaraka kwa walimu na kuwa na utawala
bora kisha kutekeleza mapendekezo ya wakaguzi ikiwa ni pamoja na kutatua
kero za walimu kadri ya uwezo utakavyoruhusu”.Alisema
Aidha
aliongeza kuwa mikakati mingine ni kufanya tafiti za kielimu kubaini kero ili
kuzifanyia ufumbuzi kwa kulenga kufanikisha mpango wa kitaifa wa Matokeo
Makubwa Sasa (Big Results Now).
Pamoja na
malengo hayo zilitajwa baadhi ya changamoto kuwa ni upungufu wa
miundombinu ya kufundishia na kujifunzia hasa vyumba vya madarasa 798 ili
kukidhi mahitaji ya vyumba 1415 kupunguza msongamano wa wanafuzi katika
darasa moja.
Upungufu
mwingine ni nyumba 962 za walimu kwani walimu wanne hukaa katika nyumba
moja huku wanafuzi wakihitaji kuongezewa matundu ya vyoo 873 na
yaliyopo ni 1085 kwa wastani wanafunzi 47 hutumia tundu moja badala
ya wafafuzi 25.
Hata hivyo
mgeni rasmi katika maadhimisho hayo mkuu wa wilaya ya Biharamulo Richard
Mbeho aliwashauri viongozi wa idara ya elimu na kata ya Nyamigogo
wilayani humo kutobweteka na ufaulu walioupata mwaka jana kuepuka kurudi nyuma
kitaaluma.
Alisema
uongozi wa elimu kwa kushirikiana na ofisi za mipango katika halmashauri
ya wilaya hiyo baadhi ya changamoto zinaweza kutafutiwa ufumbuzi kama
kutakuwepo ushirikishaji wa jamii hasa ukusanyaji wa vifaa vinavyopatikana kwa
wananchi.
Viongozi
mbalimbali wilayani Biharamulo waliohudhuria kilele cha wiki ya elimu katika
shule na kata ya Nyamigogo walifanya zoezi la upandaji miti katika shule ya
Nyamigogo.
Na:- Shaaban
Ndyamukama –BIHARAMULO.
No comments:
Post a Comment