MVUA:-Hii ndio Taswira ya Abiria wa Mikoani wakikwama baada ya Daraja la Ruvu -Barabara ya Dar Es Salaam-Morogoro kujaa Maji kutokana na Mvua zinazonyesha Nchini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 14, 2014

MVUA:-Hii ndio Taswira ya Abiria wa Mikoani wakikwama baada ya Daraja la Ruvu -Barabara ya Dar Es Salaam-Morogoro kujaa Maji kutokana na Mvua zinazonyesha Nchini.

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini mbali na kusababisha vifo na maafa mengine, pia madaraja muhimu katika barabara yamebomoka kutokana na athari za mvua hizo, njia kuu za kuingia Dar es Salaam, ikiwamo barabara za Morogoro, Bagamoyo na Kilwa zilifungwa (April 13,2014) na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wasafiri.

Wakati Rais Jakaya Kikwete alikwenda kutembelea maelfu ya abiria waliokwama kwenye daraja la Ruvu, wakielekea mikoa mbalimbali baada ya kukwama kutokana na Daraja la Ruvu, kujaa maji ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini…ambapo Akizungumza na maelfu ya abiria waliokwama tangu alfajiri huku wengine wakiwa wamekwama tangu jana usiku, Kikwete alisema ni mara yake ya kwanza kuona mafuriko kwenye eneo hilo, ambalo liko kwenye mkondo wa mto Ruvu.


 Maeneo yaliyoharibika ni karibu na Daraja la Mto Ruvu lililofurika maji na kusababisha magari kwenda mikoa ya Kaskazini, Magharibi na Nyanda za Juu Kusini na nchi jirani kukwama.


Wasafiri kutoka mikoani kuelekea jijini Dar es Salaam, waliokuwa wakisafiri jana wakiwa eneo la Ruvu Darajani wakitafakari jinsi ya kuvuka eneo hilo baada ya barabara kujaa maji na kushindwa kuvuka kwa mabasi kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.


Baadhi ya magari yaliyokwama kuvuka eneo hilo yakiwa katika msongamano huku kukiwa na usimamizi wa askari polisi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad