LA LIGA 2013/2014:-Atletico Madrid sasa wanahitaji Pointi 6 tu katika Mechi zao 3 zilizobaki ili wawe Mabingwa wapya wa La Liga . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 28, 2014

LA LIGA 2013/2014:-Atletico Madrid sasa wanahitaji Pointi 6 tu katika Mechi zao 3 zilizobaki ili wawe Mabingwa wapya wa La Liga .

Wachezaji wa Atletico Madrid wakishangilia ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Valencia jana (April 27,2014), kwa bao pekee la mchezaji Raul Garcia dakika ya 43 na kuwafanya wajiimarishe kileleni mwa La Liga na sasa wanahitaji Pointi 6 tu katika Mechi zao 3 zilizobaki ili wawe Mabingwa wapya wa La Liga kwa msimu wa mwaka 2013/2014.
Huko uwanja wa  Estadio de Mestalla, Vinara wa La Liga, Atletico Madrid wameifunga Valencia Bao 1-0 na kujiimarisha kileleni wakiwa Pointi 88 ,sawa na Pointi 4 mbele ya Timu ya Pili, FC Barcelona iliyoshinda bao 3-2 dhidi ya Villarreal na kufikisha Pointi 84 huku Real Madrid ikibaki nafasi ya tatu kwa kuwa na Pointi 82 kwa michezo 34.

Atletico Madrid Jumatano (April 30,2014) wanasafiri kwenda Stamford Bridge kurudiana na Chelsea kwenye Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, wanahitaji Pointi 6 tu katika Mechi zao 3 zilizobaki ili wawe Mabingwa wapya wa La Liga kwa msimu wa mwaka 2013/2014.

Bao la Atletico lilifungwa na Raul Garcia katika Dakika ya 43 kwa Kichwa alipounganisha Krosi ya Gabi.

Atletico Madrid walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 wakati Mchezaji wao Juanfran alipopewa Kadi Nyekundu kwa Rafu mbaya katika Dakika za Majeruhi.


Nyota wa Atletico Madrid, Raul Garcia
akishangilia bao lake pekee.
  • Valencia CF 0 - 1 Atlético Madrid 
  • Villarreal 2 - 3 Barcelona 
  • Espanyol 1 - 2 Almería 
  • Athletic Bilbao 3 - 1 Sevilla 
Position Team Played Goal Difference Points
1 Atlético Madrid 35 53 88
2 Barcelona 35 67 84
3 Real Madrid 34 66 82
4 Athletic Bilbao 35 24 65
5 Sevilla 35 16 59
6 Real Sociedad 35 8 57
7 Villarreal 35 11 52
8 Valencia CF 35 -1 45
9 Rayo Vallecano 35 -26 43
10 Levante 35 -11 42
11 Espanyol 35 -7 41
12 Málaga 35 -7 41
13 Celta de Vigo 34 -11 40
14 Granada CF 35 -23 37
15 Elche 35 -19 36
16 Osasuna 35 -29 35
17 Getafe 35 -21 35
18 Almería 35 -31 33
19 Real Valladolid 33 -18 32
20 Real Betis 35 -41 22

Mon 28 Apr 2014 - Spanish La Liga
  • Celta de Vigo v Real Valladolid 21:00
Fri 2 May 2014 - Spanish La Liga
  • Rayo Vallecano v Athletic Bilbao 20:00
Sat 3 May 2014 - Spanish La Liga
  • Barcelona v Getafe 15:00
  • Málaga v Elche 17:00
  • Osasuna v Celta de Vigo 19:00
  • Real Valladolid v Espanyol 21:00
Sun 4 May 2014 - Spanish La Liga
  • Almería v Real Betis 11:00
  • Levante v Atlético Madrid 16:00
  • Sevilla v Villarreal 18:00
  • Real Madrid v Valencia CF 20:00
Mon 5 May 2014 - Spanish La Liga
  • Real Sociedad v Granada CF 21:00
Wed 7 May 2014 - Spanish La Liga
  • Real Valladolid v Real Madrid 20:00

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad