KUFUZU FAINALI ZA AFRIKA U 20:-Tanzania yaitoa Kenya kwa penati 4-3. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 27, 2014

KUFUZU FAINALI ZA AFRIKA U 20:-Tanzania yaitoa Kenya kwa penati 4-3.


Kikosi cha Timu ya soka ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes, kilichoitoa Kenya leo(April 27, 2014) katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa-Dar es Salaam,ikiwa ni mchezo wa raundi ya Kwanza ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini Senegal kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya jumla ya bila kufungana nyumbani na ugenini.
Kwa matokeo hayo, Ngorongoro inayofundishwa na kocha mzalendo John Simkoko sasa itamenyana na Nigeria katika hatua inayofuata.

Penalti za Tanzania zilikwamishwa nyavuni na Mohammed Hussein, Kevin Friday, Mange Chagula na Iddi Suleiman, wakati Mudathir Yahya alikosa.

Penalti za Kenya zilifungwa na Geoffrey Shiveka, Timonah Wanyonyi na Victor Ndinya, wakati Evans Makari na Harison Nzivo walipoteza.

Hakuna kipa aliyeokoa penalti bali wapigaji waliokosa walipiga nje.

Ilikuwa mechi kali na ya ushindani na makipa wa timu zote mbili, Aishi Manula wa Tanzania na Farouk Shikhalo wa Kenya aliyeanza kabla ya kumpisha Boniface Barasa dakika ya 88 walifanya kazi nzuri ya kuokoa michomo ya hatari. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad