EPL 2013/2014:-Chelsea yatoa pigo Kubwa kwa Liverpool na kuondoa ndoto yao ya kutwaa Ubingwa wao wa kwanza katika Miaka 24 . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 27, 2014

EPL 2013/2014:-Chelsea yatoa pigo Kubwa kwa Liverpool na kuondoa ndoto yao ya kutwaa Ubingwa wao wa kwanza katika Miaka 24 .

Chelsea wamewapa pigo kubwa Liverpool na ndoto yao ya kutwaa Ubingwa wao wa kwanza katika  miaka 24 na wao kujiwekea matumaini baada ya kushinda Bao 2-0 katika mchezo wa Ligi kuu leo April 27,2014,Uwanjani Anfield wakiwa wamechezesha ‘Kikosi hafifu’ huku jicho lao likiwa kwenye Mechi yao ya Marudiano ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Jumatano April 30,2014 kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Mashabiki wa Liverpool walikusanyika kwa ajili ya Mechi hii wakiwa na hakika ya ushindi, hasa baada Jose Mourinho kudokeza atachezesha ‘Kikosi hafifu’, na kabla ya Mechi kuanza Basi lililobeba Wachezaji wa Liverpool lilipokuwa kwa shangwe kubwa nje ya Anfield mithili ya Paredi ya Ubingwa.
Bao zilizoiua Liverpool zilifungwa na Demba Ba katika Dakika ya 45 baada ya Nahodha Steven Gerrard kuteleza na Demba Ba kunufaika na kwenda kufunga na la Pili kupigwa Dakika za Majeruhi na Willian, alietokea Benchi, alipopokea Pasi murua ya Fernando Torres.


Ushindi huu umewaacha Chelsea wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Liverpool lakini huenda matokeo haya yakawanufaisha sana Manchester City ambao wana Mechi mbili mkononi na wakishinda zote wataikamata Liverpool na kuongozaa kwa Ubora wao wa Magoli.


Position Team Played Goal Difference Points
LIGI KUU UINGEREA 2013/2014 RATIBA.

[Saa za Bongo]
Jumatatu 28 Aprili 2014

2200 Arsenal v Newcastle

Jumamosi 3 Mei 2014

1445 West Ham v Tottenham
1700 Aston Villa v Hull
1700 Man United v Sunderland
1700 Newcastle v Cardiff
1700 Stoke v Fulham
1700 Swansea v Southampton
1930 Everton v Man City

Jumapili 4 Mei 2014

1530 Arsenal v West Brom
1800 Chelsea v Norwich

Jumatatu 5 Mei 2014

2200 Crystal Palace v Liverpool

Jumanne 6 Mei 2014

2145 Man United v Hull

Jumatano 7 Mei 2014

2145 Man City v Aston Villa
2145 Sunderland v West Brom

Jumapili 11 Mei 2014
[Mechi zote Saa 1700]

Cardiff v Chelsea
Fulham v Crystal Palace
Hull v Everton
Liverpool v Newcastle
Man City v West Ham
Norwich v Arsenal
Southampton v Man United
Sunderland v Swansea
Tottenham v Aston Villa
West Brom v Stoke


1 Liverpool 36 50 80
2 Chelsea 36 43 78
3 Man City 35 57 77
4 Arsenal 35 21 70
5 Everton 36 21 69
6 Tottenham 36 3 66
7 Man Utd 35 20 60
8 Southampton 36 7 52
9 Newcastle 35 -15 46
10 Stoke 36 -11 44
11 Crystal Palace 36 -14 43
12 Swansea 36 -1 39
13 Hull 35 -9 37
14 West Ham 36 -11 37
15 West Brom 35 -12 36
16 Aston Villa 35 -17 35
17 Sunderland 35 -20 32
18 Norwich 36 -32 32
19 Fulham 36 -42 31
20 Cardiff 36 -38 30

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad