Meli hiyo
ilikuwa na watu 460. Zaidi ya miatatu hawajapatikana , wengine 164 wameokolewa
na wengine wawili wamethibitishwa kufariki.
|
Wanafunzi
wengi waliokolewa kupitia mashimo yaliyo kando ya meli hiyo huku wengine
wakiruka baharini katika jitihada za kuokoa maisha yao.
|
"watu walikuwa wakihangaika kukimbilia maeneo ya juu ya meli, lakini ilikuwa vigumu kufanya hivyo kutokana na meli kupinduka."..Bado haijafahamika kilichosababisha… |
Watu wawili
wameripotiwa kufariki ingawa shughuli ya uokozi ingali inaendelea. Wengine
zaidi ya miatatu bado hawajulikani waliko.
|
Zaidi ya
watu miatatu bado hawajapatikana baada ya meli iliyokuwa imewabeba wanafunzi
kuzama nchini Korea Kusini.
Awali
maafisa walikuwa wamesema kuwa wengi wa abiria waliokuwa katika meli hiyo
waliokolewa.
Baadhi ya
walionusurika wamekuwa wakielezea hali ilivyokuwa ya kutisha ndani ya meli
ilipoanza kusimama kwa kuyumba, ikiegemea upande mmoja na haraka kuanza kuzama.
Bado
haijafahamika kilichosababisha kuzama kwa meli hiyo, ambayo kwa kiasi kikubwa
iliwabeba wanafunzi wa shule, lakini watu walionusurika katika ajali hiyo
wanatoa maelezo sawa kuhusu tukio hilo la kutisha.
Kikosi cha
Walinzi wa Pwani ya Korea Kusini kimesema abiria wapatao mia tatu hawajulikani
walipo baada ya meli kupinduka na kuzama.
Watu wawili
wamefahamika kupoteza maisha na watu mia moja na sitini na wanne wameokolewa.
Wengi wa
abiria wa meli hiyo walikuwa wanafunzi wa sekondari wakiwa katika safari ya
masomo kuelekea kisiwa cha Jeju, nchini Korea Kusini.
Meli hiyo
ilikuwa na watu 460. Zaidi ya miatatu hawajapatikana , wengine 164 wameokolewa
na wengine wawili wamethibitishwa kufariki.
Chanzo:-BBC-Swahili.
No comments:
Post a Comment