Jeshi la polisi wilayani Kakonko limesema kuwa waliouwawa ni mwanaume mmoja pamoja na mwanamke mmoja ambao hawakujulikana majina yao mara moja na miili yao iko katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Kakonko .
Aidha jeshi
hilo limebainisha kuwa dereva wa gari hilo Bw.Adrof Sadock ametoroka baada ya
kutokea kwa ajali hiyo na mpaka sasa hajulikani aliko .
Baada ya
kutokea kwa ajali hiyo basi moja ambalo lilikuwa nyuma ya gari hiyo iliyopata
ajali liliwachukua majeruhi wote na kuwakimbiza katika hospitali ya wilaya ya Kibondo
kwa matibabu zaidi.
Mganga mfawidhi
wa hospitali ya wilaya ya Kibondo,Dr.Frolian Tinuga amekili kupokea majeruhi
hao 13 na kwamba hali zao zinaendelea vizuri na wanaendelea na matibabu.
Baadhi ya majeruhi
waliokuwemo katika gari hilo wameelezea chanzo cha ajali hiyo wakisema kuwa ni
mwendo kasi na kwamba taili la nyuma lilipata pancha hivyo gari liliyumba sana
na kusababisha kuanguka na kubinuka mara kadha.
Jeshi la Polisi
wilaya ya Kakonko limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba ajali hiyo
imehusisha gari aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T 498 CSM na kwamba
upelelezi zaidi wa tukio hilo bado unaendelea.
Habari Na:-James Jovin-Kibondo.






No comments:
Post a Comment