AJALI:- Basi la abiria la Kampuni ya Magu Logistics lapata ajali eneo la Busiri na watu 9 kujeruhiwa leo(April 10,2014). - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, April 10, 2014

AJALI:- Basi la abiria la Kampuni ya Magu Logistics lapata ajali eneo la Busiri na watu 9 kujeruhiwa leo(April 10,2014).


Watu 9 wamefikishwa katika Hospitali Teule ya wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera, kwa ajili ya kutibiwa majeraha mbalimbali baada ya basi la abiria la Kampuni ya Magu Logistics walilokuwa wakisafiria kutoka wilayani Ngara kwenda Jijini Mwanza kupata ajali leo(April 10,2014)...Picha na Maktaba Yetu.


Ajali hiyo iliyohusisha basi la abiria la Kampuni ya Magu Logistics lenye namba za usajili T 947 ACN imetokea leo(April 10,2014) asubuhi katika eneo la Busiri wilayani Biharamul,mkoani Kagera wakati likiwa njiani kutoka wilayani Ngara kwenza Jijini Mwanza.

Mmoja wa majeruhi hao Bi Ashura Isack amesema kuwa basi walilokuwa wakisafiria limegongwa na Lori la Mizigo ambalo halijafahamika namba zake hali iliyosababisha kuacha njia na kupinduka.

Aidha Muuguzi mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Biharamulo,Sister Thea Joseph amesema kuwa kati ya majeruhi waliofikishwa Hospitalini hapo, 6 ni wanawake na wanaume ni watatu ambapo wawili wametibiwa na kuruhisiwa na kwamba hakuna aliyefariki na kufikishwa kwenye hospitali hiyo kutokana na ajali ya basi hilo.

Habari Na:-Radio Kwizera FM.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad