Klabu ya
Real Madrid imetwaa Kombe la Mfalme(Copa del Rey) baada ya kuichapa FC Barcelona
mabao 2-1 usiku huu(April 17, 2014) katika Uwanja wa Mestala mjini Valencia,
Hispania.
Real Madrid walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 10, mfungaji akiwa ni Angel di Maria akimalizia pasi ya Karim Benzema, lakini Bartra akaisawazishia Barcelona dakika ya 68.
![]() |
Bale akishangilia bao lake
dk 85 katika
ushindi wa 2-1.
|
Barcelona,
ambao wameshatwaa Kombe hilo mara 26, mara ya mwisho kulitwaa ni 2012, wakati
Real Madrid , ambao wamelitwaa mara 19 sasa, Mwaka Jana 2013 walifungwa Fainali
na Atletico Madrid.
Baada ya
kunyakua taji la kwanza msimu huu 2013/2014, Real Madrid sasa inaelekeza nguvu
zake katika mataji mengine mawili, La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya ambako
imefika hatua ya Nusu Fainali na itamenyana na mabingwa watetezi, Bayern
Munich.
Kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Hispania, Real Madrid inachuana na Atletico Madrid walio kileleni na Barcelona walio nafasi ya tatu.
No comments:
Post a Comment