![]() |
|
Hapa waendesha
pikipiki wakiwa katika kituo cha mafuta-sheri wakijaza fultank –mafuta wakijiaanda
kwenda kumtafuta hapa ni sheri ya Mashaka Stand mpya…Picha Na mdau:- Jerome
Dickson-Kibondo
|
![]() |
|
Wanachama
251 wa Chama cha Bodaboda wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wakiwa Maeneo ya Makondeko, Kibondo mjini tayari kwa safari ya kuelekea kuusaka Mwili wa
marehemu na hatimae kuupata.
|
![]() |
|
Msafara wa Wanachama
wa Chama cha Bodaboda wilayani Kibondo
Mkoani Kigoma ukiwa njiani Kwenda Mazishini katika makaburi ya Nabuhima
wilayani humo.
|
![]() |
|
Msafara wa Wanachama
wa Chama cha Bodaboda wilayani Kibondo
Mkoani Kigoma ukiwa njiani Kwenda Mazishini katika makaburi ya Nabuhima
wilayani humo.
|
Wanachama
251 wa Chama cha Bodaboda wilayani Kibondo Mkoani Kigoma kwa kushirikiana na Jeshi
la Polisi wamefanya msako na kufanikiwa kumpta mwendesha pikipiki mwenzao Bw
Idrisa Richard akiwa tayari ameuawa na mwili wake kutelekezwa porini.
Marehemu amezikwa
leo April 03,2014,Katika makaburi ya Nabuhima wilayani humo.
Akizungumza
katika eneo la tukio Mwenyekiti wa Chama hicho Bw Elisha Msigwa amesema kuwa Bw
Richard ameepotea tangu March 29 ,mwaka huu majira ya saa moja usiku wakati
amebeba abiria wawili waliokuwa wakielekea kijiji cha Nyagwijima.
Amesema kuwa
wamempata mwenzao huyo akiwa ameuawa kwa kupigwa na kunyongwa na kamba na kisha
kuporwa pikipiki yake na vitu vyote alivyokuwa navyo.
Kwa upande
wake Mkuu wa Upelelezi toka Jeshi la Polisi wilayani Kibondo Bw James Ntandu
amesema kuwa zoezi la kuwatafuta watuhumiwa wa mauaji hayo linaendelea ambapo
ametoa wito kwa wakazi wa wilaya hiyo kutoa taarifa kuhusu watu wanaohisiwa
kuhusika ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Habari
Na:-Radio Kwizera FM.















No comments:
Post a Comment