EPL 2013/2014:-Arsenal wajikita nne bora baada ya kuwafumua Newcastle United 3-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 29, 2014

EPL 2013/2014:-Arsenal wajikita nne bora baada ya kuwafumua Newcastle United 3-0.

Arsenal wakishangilia ushindi wao Jana usiku April 28,2014 na  kuwafanya sasa wawe wamebakisha ushindi katika Mechi yao moja kati ya mbili walizobakiza ili kujihakikishia wanamaliza Nafasi ya 4 na kucheza mashindano ya Klabu Bingwa barani Ulaya Msimu ujao 2014/2015,baada ya kuifunga Newcastle Bao 3-0 huko Emirates Jijini London kwenye Mechi pekee ya Ligi Kuu Uingereza.

Bao la kwanza la Arsenal likifungwa na Laurent Koscielny dakika ya 26 , Mesut Ozil Dakika ya 42 na Olivier Giroud Dakika ya 66…na kupeleka Kipigo hicho kuwa muendelezo wa Matokeo mabaya kwa Newcastle ambao sasa wamefungwa katika Mechi zao 7 kati ya 8 walizocheza mwisho kwenye Ligi na wanabaki kwenye Nafasi yao ya 9.

Mesut Ozil akiifungia Arsenal bao la pili dakika ya 42.

Olivier Giroud akihitimisha kwa bao la nne dakika ya 66.

Mashabiki wa Newcastle wakiwa na bango la kumkataa kocha wao, Alan Scott Pardew.


Arsenal FC wamezidi kujihakikishia kubaki nafasi ya Nne Bora kwenye Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuibamiza bao 3-0 Newcastle jana usiku April 28,2014,kwenye Uwanja wa Emirates jijini London.

Mabao ya Arsenal yalifungwa kimiani na Laurent Koscielny, Mesut Ozil and Olivier Giroud.

Kwa matokeo  hayo, Arsenal wamefikisha pointi 73 baada ya kucheza mechi 36 wakiwa nafasi ya nne huku anayewafuatia kwa nyuma  na Everton akiwa na pointi 69 baada ya mechi 36 wote wakibakiwa na mechi mbili mkononi.


LIGI KUU UINGEREZA 2013/2014 RATIBA.

[Saa za Bongo]

Jumamosi 3 Mei 2014.

1445 West Ham v Tottenham
1700 Aston Villa v Hull
1700 Man United v Sunderland
1700 Newcastle v Cardiff
1700 Stoke v Fulham
1700 Swansea v Southampton
1930 Everton v Man City

Jumapili 4 Mei 2014

1530 Arsenal v West Brom
1800 Chelsea v Norwich

Jumatatu 5 Mei 2014

2200 Crystal Palace v Liverpool

Jumanne 6 Mei 2014

2145 Man United v Hull

Jumatano 7 Mei 2014

2145 Man City v Aston Villa
2145 Sunderland v West Brom

Jumapili 11 Mei 2014

[Mechi zote Saa 1700]

Cardiff v Chelsea
Fulham v Crystal Palace
Hull v Everton
Liverpool v Newcastle
Man City v West Ham
Norwich v Arsenal
Southampton v Man United
Sunderland v Swansea
Tottenham v Aston Villa
West Brom v Stoke


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad