Mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Yanga SC leo
March 22,2014 imeibuka na ushindi na mabao 3 - 0 dhidi ya wenyeji timu ya Rhino Rangers
katika mchezo uliofanyika jioni ya leo katika dimba la Uwanja wa Ally Hassan
Mwinyi mjini Tabora.
Yanga SC ambayo inapigana kuhakikisha inatete Ubingwa wake kwa mara ya pili
mfululizo, iliingia uwanjani kwa lengo la kusaka pointi 3 muhimu jambo ambalo
wamefanikiwa na kusogea nyuma ya Azam FC kwa tofauti ya pointi moja tu.
Bao za Yanga
zilifungwa na Jerry Tegete, Bao 2, na Hussein Javu.
Nako huko
Azam Complex, Chamazi, Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, Mbeya City iliwachapa
Wenyeji wao Bao 2-0 na kujizatiti Nafasi ya 3 kwenye VPL.
Bao zote za
Mbeya City zilifungwa na Saidi Kipanga.
Kwa matokeo hayo, Mbeya City wanafikisha pointi 42 katika nafasi ya
tatu, pointi moja nyuma ya Yanga wenye pointi 43 baada ya kushinda leo mabao
3-0 mjini Tabora.
Utofauti wa pointi moja unaonesha jinsi ambavyo timu za ligi kuu hasa
za juu zinaendelea kupambana kutafuta taji msimu huu.
Ligi hiyo itaendelea kesho Jumapili March 23,2014, kwa mechi nne ambapo
Simba itacheza na Coastal Union katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Azam
itaoneshana kazi na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex. Mechi hizo mbili
zitakuwa ‘live’ kupitia Azam Tv.
Mechi nyingine za kesho Jumapili ni Mgambo Shooting dhidi ya
Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, wakati Ruvu Shooting na
Ashanti United zitapimana ubavu kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani
Pwani.






No comments:
Post a Comment