VPL 2013/2014:- Azam FC na matumaini ya Ubingwa ikiwa Pointi 47 sasa huku Simba SC hoi kwa Wagosi wa Kaya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, March 23, 2014

VPL 2013/2014:- Azam FC na matumaini ya Ubingwa ikiwa Pointi 47 sasa huku Simba SC hoi kwa Wagosi wa Kaya.


Kikosi cha Simba SC kilichoanza Mchezo wa Leo March 23,2014,ambapo wekundu hao wa Msimbazi Simba SC imeendelea kusuasua katika Ligi Kuu Soka Vodacom Tanzania Bara baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Coastal Union kwa bao la Coastal kufungwa na Hamad Juma dakika ya 45 kipindi cha kwanza katika mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar.


Kikosi cha Coastal Union kilichoibuka na Ushindi dhidi ya Simba SC na Matokeo hayo yameipandisha Coastal na kukamata Nafasi ya 6 na kuiacha Simba SC ikigaagaa Nafasi ya 4 ikiwa Pointi 6 nyuma ya Timu ya Tatu Mbeya City, 7 nyuma ya Yanga na 11 nyuma ya Vinara Azam FC huku wakiwa wamebakiza Mechi 4 kumaliza Ligi.

Benchi la ufundi la Simba SC.

Benchi la ufundi la Coastal.

Katika mchezo mwingine wa Ligi hiyo.Azam FC wamefanikiwa kuwafunga bao 1-0 JKT Oljoro,kwa bao la  Dakika ya 71 la John Bocco .

Ushindi huu umeifanya Azam FC ipae kileleni ikiwa na Pointi 47 kwa Mechi 21 na kuiacha Yanga ikiwa Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 43 kwa Mechi 20.

MSIMAMO.

NA TIMU P W D L GD PTS
1 Azam FC 21 13 8 0 28 47
2 Yanga SC 20 12 7 1 22 43
3 Mbeya City 22 11 9 2 12 42
4 Simba SC 22 9 9 4 16 36
5 Kagera Sugar 21 8 8 5 3 32
6 Coastal Union 22 6 11 5 2 29
7 Ruvu Shooting 20 7 7 6 -4 28
8 Mtibwa Sugar 21 6 8 7 -1 26
9 JKT Ruvu 22 8 1 13 -15 25
10 Prisons FC 20 3 10 7 -4 19
11 Mgambo JKT 20 4 6 10 -17 18
12 Ashanti United 21 4 6 11 -18 18
13 JKT Oljoro 22 2 9 11 -17 15
14 Rhino Rangers 22 2 7 13 -17 13

RATIBA MECHI ZIJAZO ZA LIGI KUU.

Jumatano Machi 26,2014.

Mgambo JKT v Azam FC
Yanga v Tanzania Prisons

Jumamosi Machi 29,2014.

Ashanti United v JKT Oljoro

Jumapili Machi 30,2014.

Mbeya City v Tanzania Prisons
Kagera Sugar v Ruvu Shooting
Mtibwa Sugar v Coastal Union
JKT Ruvu v Rhino Rangers
Azam FC v Simba
Mgambo JKT v Yanga

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad