GHARIKA:- Jose Mourinho amempa mechi ya 1,000 chungu Arsene Wenger baada ya Chelsea kuigaragaza Arsenal mabao 6-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza Leo March 22,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, March 22, 2014

GHARIKA:- Jose Mourinho amempa mechi ya 1,000 chungu Arsene Wenger baada ya Chelsea kuigaragaza Arsenal mabao 6-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza Leo March 22,2014.


Samuel Eto'o akishangilia baada ya kuifungia Chelsea bao la kwanza Stamford Bridge Leo March 22,2014,dakika ya tano kwa pasi ya Andre Schurrle, ambaye yeye mwenyewe akafunga la pili dakika ya saba kwa pasi ya Nemanja Matic kabla ya Edin Hazard kufunga kwa penalti dakika ya 17…kwa Penalti hiyo ilifuatia Alex Oxlade-Chamberlain kuushika mpira kwa makusudi akiokoa shuti la Edin Hazard, lakini ajabu refa akampa kadi nyekundu Kieran Gibbs.

Sherehe na kumbukumbu za  kocha Arsene Wenger za kutimiza mechi 1,000 akiwa Meneja wa Arsenal leo March 22,2014, zimekuwa majanga makubwa baada ya Timu yake kutandikwa Bao 6-0 huko Stamford Bridge toka kwa Vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea, na pia kucheza muda mwingi wa Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada Kieran Gibbs kupewa Kadi Nyekundu, ambayo kama ilistahili, basi aliepaswa kupewa ni Oxlade-Chamberlain na si yeye.

Huu ni ushindi mkubwa kwa Jose Mourinho katika Ligi Kuu England na ni mara ya kwanza kwa Chelsea kuifunga Arsenal Bao 6.

Pia ni Jose Mourinho ambae aliifunga Arsenal wakati Arsene Wenger anatimiza Gemu yake ya 500 na sasa Mourinho hajafungwa na Wenger katika Gemu zote 11 walizokutana.



Bao nyingine za Chelsea zilifungwa na Oscar, Bao 2, na Mohamed Salah.

Penati hiyo ya Eden Hazard ilitolewa na Refa Andre Marriner baada Alex Oxlade-Chamberlain kuokoa Mpira kwa mkono lakini Refa huyo alifanya makosa na kumpa Kadi Nyekundu Kieran Gibbs licha ya Oxlade-Chamberlain kumwambia Refa ni yeye alieshika.

Latest Football EPL 2013/2014.

Top of Form
Bottom of Form
  • Chelsea 6 - 0 Arsenal 
  • Cardiff 3 - 6 Liverpool
  • Everton 3 - 2 Swansea
  • Hull 2 - 0 West Brom
  • Man City 5 - 0 Fulham
  • Newcastle 1 - 0 Crystal Palace
  • Norwich 2 - 0 Sunderland 
  • West Ham 0 - 2 Man Utd.... HT

Position Team Played Goal Difference Points
1 Chelsea 31 39 69
2 Liverpool 30 44 65
3 Man City 28 49 63
4 Arsenal 30 19 62
5 Everton 29 13 54
6 Tottenham 30 -1 53
7 Man Utd 30 14 51
8 Newcastle 30 -2 46
9 Southampton 30 6 45
10 Aston Villa 29 -6 34
11 Stoke 30 -12 34
12 Hull 30 -5 33
13 Norwich 31 -22 32
14 West Ham 30 -8 31
15 Swansea 30 -6 29
16 West Brom 30 -12 28
17 Crystal Palace 30 -20 28
18 Sunderland 28 -18 25
19 Cardiff 31 -32 25
20 Fulham 31 -40 24

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad