UEFA:-Chelsea na Real Madrid yazifata Bayern Munich,Atletico Madrid,Barcelona na Paris Saint-Germain Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ,Leo ni Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg ‘’ Manchester United v Olympiacos. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, March 19, 2014

UEFA:-Chelsea na Real Madrid yazifata Bayern Munich,Atletico Madrid,Barcelona na Paris Saint-Germain Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ,Leo ni Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg ‘’ Manchester United v Olympiacos.


Chelsea imefanikiwa kuifunga Galataray ya Uturuki kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jana March 18,2014,kwenye Uwanja wa Stamford Bridge London.


Mabao ya Chelsea yalifungwa na Samuel Eto’o na beki Garry Cahill na kuipa Chelsea ushindi wa jumla ya mabao 3-1 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 jijini Istambul katika mechi ya kwanza.




Cahill akiifungia Chelsea na kukamilisha ushindi wa jumla wa 3-1 na Baada ya kutolewa kwa Manchester City na Arsenal katikati ya wiki iliyopita, Chelsea sasa imejikatia tiketi ya kuingia Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa kuifunga mabao 2-0 timu hiyo ya mchezaji wao wa zamani nyota, Didier Drogba.


Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid Jana March 18,2014,katika UEFA ,ikiilaza 3-1 Schalke na sasa  Real Madrid imeungana na wapinzani wao nchini Hispania, FC Barcelona kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi huo  ambao unawafanya wasonge mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 9-2 dhidi ya Schalke ya Ujerumani. 


Mabao yaliyoipeleka Madrid Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa yamefungwa na Cristiano Ronaldo mawili dakika za 21 na 74 akifikisha mabao 41 msimu huu, na lingine limefungwa na Alvaro Morata dakika ya 75.
Madrid ilishinda 6-1 katika mchezo wa kwanza ugenini, hivyo imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 9-2.


Bao pekee la Schalke kwenye Mechi hii lilifungwa na Tim Hoogland katika Dakika ya 31.

TIMU ZILIZOTINGA ROBO FAINALI UEFA 2013/2014.

-Bayern Munich
-Atletico Madrid
-Barcelona
-Paris Saint-Germain
-Chelsea
-Real Madrid
**Bado 2.

Jumatano Machi 19,2014.

22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg [4-2]
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP [0-2]

MATOKEO YA UEFA.


Jumanne Machi 11,2014.

Bayern Munich 1 Arsenal 1 [3-1]
Atletico de Madrid 4 AC Milan 1 [5-2]

Jumatano Machi 12,2014.

FC Barcelona 2 Manchester City 1 [4-1]
Paris Saint-Germain 2 Bayer 04 Leverkusen 1 [6-1]
 
Jumanne Machi 18,2014.

Chelsea FC 2 Galatasaray Spor Kulübü 0 [3-1]
Real Madrid CF 3 Schalke 1 [9-2]

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad