Tazama Picha za Usafiri maalum kwa Wagonjwa (Ambulance) zabuniwa na kutengenezwa Jijini Mwanza-Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, March 19, 2014

Tazama Picha za Usafiri maalum kwa Wagonjwa (Ambulance) zabuniwa na kutengenezwa Jijini Mwanza-Tanzania.

Huu hapa ubunifu wa usafiri rahisi kwa huduma ya afya, yaani kusafirishia mgonjwa kutoka eneo moja kwenda jingine kwa ajili ya kupata matibabu. zimetengenezwa Jijini Mwanza(Made in Mwanza).- Vyombo hivi vya usafiri vimekuja mara baada ya serikali hivi karibuni kuagiza ambulance za magurudumu matatu kupunguza gharama ya matumizi ya mafuta. Changa moto hizo zilifanya baadhi ya mafundi wabunifu nchini kaamua kuzifanyia kazi kwa kuunda vyombo vya style hiyo vinavyolingana na mahitaji.
Ni pikipiki za miguu mitatu zenye double tyre kwa nyuma ikiwa ni kwa ajili ya usalama zikiwa katika hatua za mwisho kukamilika katika moja ya karakana zilizopo Ghana wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Nyuma kwa ndani kushoto ni kiti cha mhudumu wa afya na msindikizaji pamoja na kitanda kwaajili ya mgonjwa (kulia).
Vyombo hivi vya usafiri vyenye magurudumu matatu maalum kwa kubebea wagonjwa vimekuja mara baada ya serikali hivi karibuni kuagiza ambulance za magurudumu matatu ambazo zinasaidia kupunguza gharama ya matumizi ya mafuta na kusambaza kama msaaada maeneo ya zahanati mbalimbali hasa wilayani na vijijini, kuonekana kuwa na changamoto zake ndipo baadhi ya mafundi wabunifu nchini wakaamua kuzifanyia kazi changamoto hizo kwa kuunda vyombo vya style hiyo vinavyolingana na mahitaji.


Source:- GSENGO

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad