![]() |
|
Abiria wakiwa ndani ya ndege mpya ya Air
Tanzania aina ya CRJ-200 muda mfipi kabla ya kutua katika uwanja wa ndege
wa Songwe wakitokea Dar es Salaam.
|
![]() |
|
Abiria wakipanda ndege ya Shirika la ndege
la Air Tanzania (ATCL) aina ya CRJ-200 katika uwanja wa ndege wakimataifa wa
Songwe wakielekea Dar es Salaa. Safari hizi zitafanyika mara nne ndani ya wiki.
|
ATCL
yaanza safari za kwenda Mbeya.
Shirika
la Ndege la Air Tanzania (ATCL) Jumatatu hii lilizindua safari zake za kwenda
Mbeya kupitia uwanja mpya wa ndege wa kimataifa wa Songwe likitumia ndege yake
mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 50 ya Canada aina ya CRJ – 200.
Safari
hiyo inayochukua kadri ya saa moja kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya
itakayofanyika siku nne kwa wiki; Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili,
ililakiwa na abiria na wafanyabiashara wanaosafiria kutoka Mbeya kwenda katika
jiji la kibiashara la Dar es Salaam.
Akizungumza
katika uzinduzi wa kihistoria uliofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Songwe, Kaimu Mkurugenzi wa Biashara/Masoko wa shirika hilo Bw. Juma Boma
alisema Air Tanzania imerudi kwa kishindo katika mji ambao ni kitovu cha
biashara kwa mikoa ya nyanda za juu kusini na inayotumika
kama njia ya kuiunganisha Tanzania na nchi za Kusini mwa
Afrika, ili kupunguza adha
ya usafirina kuiunganisha sehemu ya Kusini
mwa Tanzania na mikoa mingine.
“Safari
ya Air Tanzania kwenda Mbeya iliyosubiriwa kwa muda mrefu imeanza rasmi leo
hii. Kwa kutumia ndege yetu mpya, tunatoa usafiri wa haraka na salama,
tukiiunganisha Mbeya na mikoa mingine. Kwa saa moja tu, abiria wetu wanauhakika
wa kutua uwanja wa ndege wa Songwe kutokea Dar es Salaam.
“Tumezingatia
masuala yote ya kiuchumi ili kupanga nauli tuliyoanza nayo ambayo ni kiasi cha
shilingi 150,000 kwa tiketi ya kwenda na shilingi 260,000 kwa tiketi ya kwenda
na kurudi,” alisema,” Bw. Boma.
Alisema
uzinduzi wa njia ya Mbeya ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati madhubuti
wa upanuzi wa shirika, ambao umelenga katika kuzirejesha safari zote za ndani
na za kimataifa na kufungua njia nyingine mpya.
Boma
alisema kuwa kutokana na mkakati wao ujulikanao kama go-green utalipelekea
shirika hilo la ndege la taifa kuongeza toleo jipya ya ndege nyingine mbili
zenye uwezo wa kubeba abiria 78 mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu, shirika hilo
litaongeza idadi ya safari zake katika njia zake kuu na kuongeza safari za
kimataifa.
“Kupitia
upanuzi wa safari zetu, abiria wetu watafurahia safari za kila siku kutoka Dar
es Salaam kwenda Mwanza, ikiwa muda wa kuondokea Dar ukiwa ni saa 11 jioni na
kutokea Mwanza ni saa moja usiku. Tutakuwa tukienda mwanza mara nne
kwa wiki.
Tutakuwa
pia tukisafiri kwenda Moroni nchini Comoro katika siku za Jumatatu, Jumatano,
Ijumaa na Jumamosi.
Vile vile tunatarajia kufungua njia ya Tabora – Mpanda hivi
karibuni,” alisema.
Alibainisha
kuwa shirika hilo pia limeondoa baadhi ya adhabu watozwazo abiria wanaoshindwa
kutokea wakati wa safari na wale wanaobadilisha ratiba ya safari zao, na kusema
kuwa hii itawasaidia abiria wao kutoingia gharama za ziada endapo watakumbana
na dharura mbali mbali kabla ya safari.
Mmoja
kati ya abiria aliyesafiria katika ndege hiyo kwenda Mbeya, Deogratius
Nyanshile aliipongeza Air Tanzania kwa maamuzi yake na kutoa wito kwa
watanzania kuliunga mkono shirika kwa kusafiria na Air Tanzania.
“Nawaasa
wakazi wa mkoa wa Mbeya na kanda ya kusini kwa ujumla, kuitumia fursa hii
kikamilifu iliyotolewa na shirika la Ndege la Air Tanzania,” alisema
.
Nyanshile. Ndege hiyo ya taifa, ambayo ilisimamisha huduma zake katika
mkoa huo kwa sababu ya ubovu wa uwanja wa ndege wa zamani wa
Mbeya, imerejesha safari hizo baada ya kukamilika kwa ujenzi
wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe.
Ikitumia
ndege yake aina ya Bombardier Dash-8, ATCL kwa sasa
shirika hilo linasafiri katika zaidi ya sehemu naneTanzania ikiwa
ni pamoja na Mtwara, Mwanza,
Tabora,Kigoma, Dar es Salaam, Bujumbura, Mbeya na kwendaMoroni nchini
Comoro.
Source:-GPL.











No comments:
Post a Comment