UEFA 2013/2014:-FC Barcelona, PSG na Atletico Madrid zaungana na Bingwe mtetezi Bayern Munich kutinga hatua ya Robo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, March 13, 2014

UEFA 2013/2014:-FC Barcelona, PSG na Atletico Madrid zaungana na Bingwe mtetezi Bayern Munich kutinga hatua ya Robo.

Lionel Messi akisherehekea na wachezaji wenzake baada ya kuifungia FC Barcelona bao la kwanza jana March 12,2014, na kuichapa Manchester City mabao 2-1 uwanja wa Nou Camp na kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1.


Man City sasa yaungana na Arsenal kurudi kucheza mechi zao zaLigi kuu soka Nchini Uingereza.

Usiku wa Jana March 12,2014, FC Barcelona na Paris Saint-Germain, zote zimetinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya UEFA , baada kushinda Mechi zao za Marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16, wote wakishinda 2-1, kwa FCBarcelona kumchapa Manchester  City na PSG kumpiga Bayer Leverkusen.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Camp Nou, mabao ya Barca yalifingwa na Lionel Messi dakika ya 67 na dani Alves dakika ya 90, wakati bao City lilifungwa na nahodha wake, Vincent Kompany dakika ya 89.

Man City iliyofungwa 2-0 Uwanja wa Etihad katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 Bora, ilipata pigo jana dakika ya 78 baada ya mchezaji wake, Pablo Zabaleta kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Katika mchezo mwingine, PSG nayo ilimalizia vizuri biashara baada ya kuifunga Bayer Leverkusen mabao 2-1 Uwanja wa Pac de Princes hivyo kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 6-1, baada ya awali kushinda 4-0 ugenini.

MARUDIANO UEFA 2013/2014 MATOKEO.

[Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili]

Jumanne Machi 11,2014.

Bayern Munich 1 Arsenal 1 [3-1]
Atletico de Madrid 4 AC Milan 1 [5-2]

UEFA CHAMPIONZ LIGI  2013/2014 MARUDIANO

[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]

[Saa za Bongo]

Jumanne Machi 18,2014.

22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü [1-1]
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04 [1-6]

Jumatano Machi 19,2014. 

22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg [4-2]
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP [0-2]


Hivyo sasa FC Barcelona, Paris Saint-Germain na Atletico Madrid  wanaungana na Mabingwa watetezi Bayern Munich kutinga hatua ya Robo Fainali ya UEFA .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad