Kidato cha Pili Shunga Sekondari ndio Mabingwa wa Nzoma CUP 2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, March 13, 2014

Kidato cha Pili Shunga Sekondari ndio Mabingwa wa Nzoma CUP 2014.

Kikosi cha Timu ya Kidato cha Pili ,Shunga Sekondari baada ya kutawazwa kuwa Mabingwa wa Kombe la Nzoma 2014-Kikiwa na zawadi yao ya Mbuzi-Mnyama, Mashindano hayo yalikuwa kwa Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Shunga iliyopo wilayani Ngara mkoani Kagera yaliyoanza Februari 17,2014 na kumalizika March 11,2014.

Kikosi cha Timu ya Kidato cha Pili ,Shunga Sekondari kilicho watandika bila huruma Walimu bao 3-1 kwa bao za Aniseti Musa,Philipo Emanuel na Boaz Richard na kutawazwa kuwa Mabingwa wa Kombe la Nzoma 2014, kwa Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Shunga iliyopo wilayani Ngara mkoani Kagera yaliyoanza Februari 17,2014 na kumalizika March 11,2014.
Kikosi cha Timu ya Walimu ama Staff wa Shunga Sekondari kilicho cheza mchezo wa fainali ya kuwania Kombe la Nzoma Cup 2014.
Baadhi ya Mashabiki na Wanafunzi wa Shunga Sekondari wakifatilia mchezo wa fainali ya Nzoma CUP 2014 katika uwanja wa Shule ya Msingi Murukulazo ambapo Kidato cha pili lilifanikiwa kuwafunga bila huruma Walimu bao 3-1  na kutawazwa kuwa Mabingwa wa Kombe hilo.
Mdhamini wa Ligi hiyo ya Nzoma CUP 2014,(Kushoto)Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Shunga ya wilayani Ngara-Mwl.John Nzomalarumwe pamoja na Kilanja wa Michezo Shuleni hapo Amos John wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na Mwanawamakonda Blog kuhusu mashindano hayo ambapo pamoja na mafanikio lakini yalikumbwa na uhaba wa vifaa vya michezo kama vile Mipira na Jezi kwa timu shiriki.
Baadhi ya Wanafunzi wa  Shule ya Sekondari Shunga ya wilayani Ngara wakifurahia ushindi wa Kidato cha pili kuibuka Mabingwa wa Nzoma CUP.


Mashindano ya Nzoma CUP 2014 kwa Walimu na Wanafunzi wa shule ya sekondari Shunga iliyopo wilayani Ngara mkoani Kagera hatimaye yamemalizika March 11,2014, jioni kwa fainali ya mchezo wa soka,Hand ball,Netball na Drama.

Katika mchezo wa fainali katika soka uliochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Murukulazo,uliwakutanisha timu ya Kidato cha Pili dhidi ya Timu ya Walimu ama Staff na kidato cha Pili kufanikiwa kuwatandika bila huruma Walimu bao 3-1 kwa bao za Aniseti Musa,Philipo Emanuel na Boaz Richard huku lile la Walimu ambalo ni lakufutia machozi likifungwa na Mwl.Emanuel Gashaza.

Kufuatia Ushindi huo wa 3-1, Kidato cha Pili ndio Mabingwa wa Nzoma Cup 2014 na wameondoka na zawadi ya Mbuzi-mnyama mwenye thamani ya shilingi elfu 50 huku washindi wa pili wakiwa ni Walimu walioondoka na shilingi elfu 30.

Aidha katika fainali ya mchezo wa Handball, kidato cha pili waliibuka tena mabingwa kwa kuwafunga magoli 4-2 kidato cha nne na kuondoka na zawadi ya shilingi elfu 15,katika mchezo wa netiball, Kidato cha nne wakifanikiwa kuwa Bingwa kwa kuwafunga Kidato cha tatu goli 17-10 na kuondoka na zawadi ya shilingi elfu 15 huku katika mchezo wa Drama au Maigizo fainali  iliwakutanisha kidato cha kwanza hadi cha nne na mshindi kuibuka Kidato cha tatu kwa point 258 na kuondoka na zawadi ya Kuku Jogoo lenye thamani ya shilingi elfu 15.

Nae mdhamini wa Ligi hiyo ya Nzoma-Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari shunga-Mwl.John Nzomalarumwe pamoja na kuwapongeza washiriki wote kwa kudumisha nidhamu wakati wa mashindano hayo ameelezea pia malengo ya mashindano hayo kwa mwaka huu,kuwa ni kukuza mahusiano baina ya Walimu na Wanafunzi wa shule hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad