Ubovu wa Kipande cha Barabara Nyakanazi-Rusumo chawa chanzo cha Ajali za mara kwa mara kwa Madereva wazembe. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, March 14, 2014

Ubovu wa Kipande cha Barabara Nyakanazi-Rusumo chawa chanzo cha Ajali za mara kwa mara kwa Madereva wazembe.

Hii ni Ajali ambayo imetokea March 12,2014 katika Barabara ya Nyakanazi-Rusumo, karibu na eneo la pori la Burigi ambapo kutokana na mashimo yaliyopo katika barabara hiyo ya Lami,Dereva wa Lori hilo akiwa mwendo kasi aliingia katika shimo na hivyo gari kumshinda na hatimaye kupata ajali.

Kwa mujibu wa Mashuhuda walioongea na Mwanawamakonda blog ,wamesema kuwa hakuna mtu aliepoteza maisha zaidi ya Kujeruhiwa huku wakishangazwa na kitendo cha baadhi ya Askari Polisi kukutwa muda mfupi wa ajali kutokea wakihujumu baadhi ya Mali zilizokuwa zimebebwa katika Lori hilo.


Katibu Tawala Msaidizi, Idara ya Miundombinu mkoani Kagera Bw Seif Hussein amesema serikali inaendelea kufanya ukarabati wa barabara ya Isaka - Rusumo kwa kuwa imeanza kuharibika kutokana na kujengwa zaidi ya mika 30 iliyopita.

Bw Hussein amesema hayo March 12,2014, wakati akizungumza na Radio Kwizera wilayani Ngara mkoani Kagera, kufuatia malalamiko ya wananchi kuhusu kipande cha barabara kutoka Nyakanazi, Biharamulo hadi Rusumo wanachodai kuwa kero kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Amesema kuwa barabara hiyo hutumika kusafirisha mizigo mizito ndani na nje ya nchi hali inayosababisha baadhi ya maeneo kuharibika na kwamba barabara hiyo ilitakiwa kufanyiwa ukarabati wa kudumu baada ya miaka 20 lakini tatizo ni upatikanaji wa fedha

Hata hivyo Mkuu wa mkoa wa Kagera ,Kanali mstaafu Fabian Masawe amewataka watumiaji wa barabara hiyo kuitumia kwa umakini katika kusafirisha abiria na mizigo na kwamba changamoto za barabara zitapungua baada ya kukamilika kwa ujenzi wa reli ya kusafirisha mizigo.

Habari Na:-Radio Kwizera FM.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad