TAZAMA PICHA::Wajumbe Bunge Maalum la Katiba wakiapishwa wiki hii Mjini Dodoma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, March 15, 2014

TAZAMA PICHA::Wajumbe Bunge Maalum la Katiba wakiapishwa wiki hii Mjini Dodoma.


Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Samwel Sitta akila kiapo mbele ya  Katibu wa Bunge hilo Bw. Yahya Khamis Hamad, wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Jana March 14,2014,Mjini Dodoma.Kulia ni Naibu Katibu wa Bunge Hilo Thomas Kashilila.

Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samia Suluhu Hassan akila kiapo mbele ya Naibu Katibu wa Bunge Hilo Thomas Kashilila, wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.Kulia ni Katibu wa Bunge Hilo Yahya Khamis Hamad.


Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye ni Mwanasheria Mkuu Frederick Werema akitoa hoja wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Jana March 14,2014, Mjini Dodoma.


Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo Pandu Ameir Kificho akila kiapo cha kuwa Mjumbe wa Bunge Hilo Mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta.


Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda akila kiapo cha kuwa Mjumbe wa Bunge Hilo Mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta.


Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Edward Lowassa akila kiapo cha kuwa Mjumbe wa Bunge Hilo Mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta.

Aidha  wajumbe hao zaidi ya 615 wa Bunge maalum la katiba jana March 14,2014, wameanza kula viapo tayari kwa kuanza rasmi shughuli ya kujadili rasimu ya katiba mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo  siku ya Jumatatu March 17,2014, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba atawasilisha rasimu ya katiba katika Bunge hilo, ambapo siku ya Jumatano Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania atalihutubia kisha kulizindua Bunge hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad