Tazama taswira ya Nyumba ikiteketea kwa Moto ,wilayani Misungwi mkoani Mwanza:-Chanzo Jiko la Gesi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, March 07, 2014

Tazama taswira ya Nyumba ikiteketea kwa Moto ,wilayani Misungwi mkoani Mwanza:-Chanzo Jiko la Gesi.

Moto ukipamba moto na kutokea kwenye madirisha ukivuma na Moto huo unaotajwa chanzo chake kusababishwa na jiko la gesi ulilipuka na kuiteketeza kabisa nyumba hiyo ikiwa na furniture zake.

Mwananchi juu ya paa la nyumba ya mtu mmoja maarufu kwa jina la Mama Mayunga, akijaribu kurusha vifuko vya mchanga katika moja ya majengo ya nyumba iliyozuka moto Jana majira ya saa 5 asubuhi mtaa wa Majengo jirani na Masangwa Guest House wilayani Misungwi mkoani Mwanza. 
Moto huo unaotajwa chanzo chake kusababishwa na jiko la gesi ulilipuka na kuiteketeza kabisa nyumba hiyo ikiwa na furniture zake.
Hali ndiyo ilivyokuwa huku wananchi hao wa wilaya ya Misungwi wakisubiri huduma ya zimamoto toka magari ya Halmashauri ya jiji la Mwanza, umbali wa dakika 45.
Huku baadhi yao wakiwa wamejitosa kufanya uokoji wa mali, wananchi wengine kama kawaida yao walikimbilia  eneo la ajali kushuhudia moto huo uliokuwa ukivuma kuashiria hatari na eneo hilo si salama. 
Ingawa jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kuwasihi wananchi kusogea mbali toka eneo la moto kwani chanzo chake ni moto wa gesi, katu watu hao hawakutii amri  hiyo zaidi ya kuusogelea zaidi.
Saa moja baadaye gari la zimamoto lilifika eneo la ajali ya moto lakini hata hivyo liliambulia kuzima magofu huku milango, madirisha na mali zilizokuwa kwenye nyumba hiyo zikiteketea kabisa. 
(Picha na Wiliam Bundala wa kanda ya Ziwa)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad