Na:- Karoli Vinsent
Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) imevipa onyo
kali televisheni ya Itv na Startv pamoja na RadioFree,kutokana na kurusha Tangazo ambalo
linakwenda kinyume na Maadili.
Hayo,yalisemwa leo March 07,2014,Jijini Dar es Salaam katika
mkutano na Waandishi wa Habari na Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui
ya Mamlaka hiyo,Margaret Mnyagi ambapo alisema Kamati imefikia maamuzi hayo
baada ya kushauriana na Kamati Maudhui ya vipindi vya Runinga vya mamlaka hiyo.
“Tumefika maamuzi haya baada ya kukaa sisi kama
kamati ya Maudhui na kubaini tangazo la Policy Forum ambalo tangazo hilo
linachochoe watu wasilipekodi,Tangazo hilo lilirushwa kwenye Runinga mbili
ambazo ni Itv pamoja na Startv na redio ambayo ni Radio Free”
“Napenda kuwatoa hofu wananchi kuwa atuchafanya
upendeleo wowote katika kutoa hukumu hii”alisema Mnyagi
Aidha Mamlaka hiyo imevitaka vyombo hivyo
vilivyorusha Tangazo hilo viwasilishe mwongozo wa urushaji wa Matangazo hayo,na
pia Mamlaka hiyo imevionya vyombo hivyo
kutorudia kuonyesha Matangazo ya Uchochezi na endapo watakaidfi Mamlaka hiyo
itawachukulia hatua kali za kisheria.
Kwa upande wake Meneja wa Mipango na Utafiti wa
Sahara Media Bw. Nassani Lwehabula ambao ni wamiliki wa
Star tv,Kiss fm,Radio free,Gazeti la Msanii wa Afrika alisema wao wamechukulia
Hukumu hiyo ni kama Changamoto kwao ya kufanya Vipindi vyao kuwa na umakini ili
waweze kukuza maudhui yao,
Ikumbukwe Tangazo liloifanya Mamlaka ya Mawasiliano
nchini kuchukua Maamuzi hayo ni Tangazo la Taasisi isiyokuwa ya kiSerikali
inayojulika PolcyForum,ambapo katika Tangazo hilo linawahamasisha wananchi
wasilipe kodi mwenzi Januari Mwaka huu.






No comments:
Post a Comment