Manchester United kufungwa bao 3-0 na Liverpool,Yapoteza mashabiki Laki 4 na Nusu katika ukurasa wao wa Facebook. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, March 18, 2014

Manchester United kufungwa bao 3-0 na Liverpool,Yapoteza mashabiki Laki 4 na Nusu katika ukurasa wao wa Facebook.


Siku ya kufa nyani, miti yote huteleza, hakuna kitu kizuri kama kushabikia mpira hasa inapotokea timu unayoipenda ikiwa inafanya vizuri kwa kuzikabili na kuzifunga timu pinzani, lakini hugeuka kuwa shubiri endapo timu hiyo ikianza kuwa shamba la bibi ama si jamvi la wageni kwa kufungwa mechi za nyumbani na nje na kuwapa nafasi wapinzani kuteleza kwa ganda la ndizi.


Hayo ndiyo yaliyokikuta kikosi cha mashetani wekundu, Manchester United baada ya kupokea vibano mfululizo kutoka kwa timu pinzani, hali iliyosababisha mashabiki wake wapatao 450,000 kujiondoa(Unlike) katika page ya timu hiyo kwenye mtandao wa Facebook baada ya kukatishwa tamaa  kwa kukubali kufungwa dimbani kwao ‘Old Trafford’  jumla ya mabao 0 -3 dhidi ya Mahasimu wao wakubwa Liverpool kwenye Ligi Kuu England na kuwaacha wakiwa Pointi 18 nyuma ya Vinara Chelsea na hivyo kuwa kwenye hali isiowezekana kutetea tena Taji lao la Ubingwa Msimu huu 2013/2014.

Pamoja na hayo Meneja wa Man United ,DAVID MOYES amesisitiza kwamba ana uhakika nafasi yake kama Meneja wa Manchester United haina wasiwasi licha ya Klabu hiyo kusuasua katika Msimu wake wa kwanza na Magazeti kadhaa huko Uingereza kutabiri kufukuzwa kwake.

Pia, Msimu huu, katika Mechi 14 za Ligi walizocheza kwao Old Trafford, Man United wamefungwa Mechi 6 kati ya 14.

Wakiwa wanakabiliwa na Mechi ya Marudiano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na Olympiakos ya Ugiriki Jumatano March 19, 2014,Usiku ambayo wanatakiwa kupindua kipigo cha Bao 2-0 ili wao wasonge mbele, Moyes, akihojiwa na Wanahabari ikiwa kushindwa kuitoa Olympiakos kutaathiri hatima yake Man United, alijibu: “Hatima yangu haijabadilika hata chembe! Nina kazi nzuri! Najua mwelekeo upi nakwenda!”

Inaaminika Bodi ya Man United, kwa sasa, haifikirii kumbadili David Moyes licha ya kufanya vibaya mno wakiwa Nafasi ya 7 kwenye Ligi huku wakibakiwa na Mechi 7.

Akizungumza na Wanahabari kwenye Mahojiano hii Leo, Moyes amesema ana sapoti kubwa ya Viongozi wa Man United akiwemo Sir Alex Ferguson ambae ndie amemrithi.

Moyes aliongeza: “Hii ni Klabu ambayo Dira yake ni ya muda mrefu, si muda mfupi na ndio maana nimepewa Mkataba wa Miaka 6!”

Hii Leo March 18, 2014, huko Uingereza, Magazeti yalipambwa na habari kuwa Moyes amepewa Siku 10 za kufanya vizuri ambapo watakuwa na Mechi 3, dhidi ya Olympiakos, West Ham na Man City, la sivyo kibarua hana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad