Tazama Picha za timu ya Ngara stars ilipocheza na Polisi Muyinga nchini Burundi March 23,2014 na kuilazimisha kutoka nayo sare ya kufungana bao 1-1 . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, March 24, 2014

Tazama Picha za timu ya Ngara stars ilipocheza na Polisi Muyinga nchini Burundi March 23,2014 na kuilazimisha kutoka nayo sare ya kufungana bao 1-1 .

Timu ya Ngara stars ya Wilaya ya Ngara ,mkoani Kagera iliyoundwa kama Kombaini na kusafiri hapo Jana March 23,2014,Jumapili kwenda mkoani Muyinga nchini Burundi kuchezana na timu ya mkoa huo ya Polisi,hatimae iliwashangaza wana Muyinga baada ya kuichomolea bao moja la timu ya Polisi inayosifika kwa kuzifunga timu pinzani za mkoa huo na kuilazimisha kutoka nayo sare ya kufungana bao 1-1.

Mashabiki wa soka toka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Muyinga nchini Burundi wakifatilia mchezo  huo wa kirafiki wa kimataifa katika kukuza masula ya ujirani mwema ,ulichezwa katika uwanja wa Jeshi wa Mukoni mjini Muyinga na Amisi Selkemaini kuiandikia bao la kwanza-timu yake ya Polisi dk 13 huku Ngara Starz wakichomoa kunako dk ya 33 kipindi cha pili.
Kikosi cha Ngara Stars kutoka wilayani Ngara mkoani Kagera kikiwa katika Picha ya Pamoja kabla ya kuanza mchezo wake dhidi ya timu ya Polisi Muyinga jana March 23,2014, mchezo  huo wa kirafiki wa kimataifa ulichezwa katika uwanja wa Jeshi wa Mukoni mjini Muyinga.
Kikosi cha Polisi Muyinga ya nchini Burundi kikiwa katika Picha ya Pamoja kabla ya kuanza mchezo wake dhidi ya timu ya Ngara Stars kutoka wilayani Ngara mkoani Kagera,nchini Tanzania jana March 23,2014, mchezo  huo wa kirafiki wa kimataifa ulichezwa katika uwanja wa Jeshi wa Mukoni mjini Muyinga.
Wachezaji wa timu zote mbili wakipita kusalimiana kabla ya kuanza mchezo ambapo timu hizo zilifungana bao 1-1, mchezo  huo ukiwa wa kirafiki wa kimataifa ulichezwa katika uwanja wa Jeshi wa Mukoni mjini Muyinga.
Baadhi ya mashabiki wa timu ya  Ngara Stars walisafiri na timu hiyo kutoka Ngara hadi Muyinga kuishangilia timu yao na uchache wao uwanjani uliwashangaza wana Muyinga ambao walijitokeza kwa wingi kushuhudia mechi hiyo.
Hivi ndivyo wananchi wa mkoa wa Muyinga nchini Burundi wanavyopenda mchezo wa soka na hapa walijitokeza kwa wingi sana  jana March 23,2014,kutazama mchezo kati ya Ngara Stars dhidi ya timu yao ya Polisi katika  mchezo  huo wa kirafiki wa kimataifa ulichezwa katika uwanja wa Jeshi wa Mukoni mjini Muyinga.
Benchi la ufundi la  timu ya Polisi Muyinga na wa kwanza kulia ni Kocha wao Ngabo Jomed akifatilia mchezo huo jana March 23,2014,  katika uwanja wa Jeshi wa Mukoni mjini Muyinga.
Benchi la ufundi la  timu ya Ngara Stars na wa tatu kutoka  kulia ni Kocha wao Baraka Abbas akifatilia mchezo huo jana March 23,2014,  katika uwanja wa Jeshi wa Mukoni mjini Muyinga.
Wa kwanza kutoka kulia ni Salumu Bakari ambae ni Afisa Michezo na Utamaduni wilaya ya Ngara,Bahati Kunzi ambae ni Kaimu katibu mkuu wa chama cha soka Ngara NDFA,Mwanasheria wa Halmshauri ya wilaya ya Ngara,Joa Katanga ambae ni katibu mkuu wa chama cha soka NDFA na Niniani Bakari ,Diwani viti maalumu na Mdau mkubwa wa michezo wilayani Ngara hususani soka la Wanawake walisafiri na Ngara Stars kuhakikisha inafanya vyema katika mchezo huo jana March 23,2014.
Baadhi ya Viongozi wa mkoa wa Muyinga na watatu toka kulia ni Afisa wa Jeshi la Polisi mkoa wa Muinga nchini Burundi, Murike Patrisi licha ya kufurahia mchezo huo lakini amesisitiza wilaya ya Ngara mkoani Kagera-Tanzania  na mkoa wa Muyinga kuzidisha kutembeleana kila mara ili kukuza ujirani mwema sambambana na mahusiano yenye Amani na Upendo
Hawana nao ni wadau wakubwa wa soka walinaswa na camera yetu wakifatilia kwa ukaribu mchezo huo ambao Ngara Stars walitoka sare ya 1-1 na Polisi Muyinga.
Ugeni kutoka wilayani Ngara mkoani Kagera nchini Tanzania ulipokelewa vizuri na kupatia huduma nzuri ya chakula.
Muonekano wa msafara wa timu ya Ngara Stars ukiwa katika Ofisi za Uhamiaji mjini Kabanga nchini Tanzania tayari kwa kusubiri taratibu za kuvuka kwenda mkoani Muyinga nchini Burundi jana March 23,2014, zikamilishwe.
Baada ya mchezo kukamilika kwa matokeo ya sare ya 1-1 ,msafara wa timu ya Ngara Stars ulianza safari yao ndefu ya kutoka  mkoani Muyinga nchini Burundi kurudi Mjini Ngara jana March 23,2014, kama unavyoona katika picha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad