MGOMO WA MADEREVA MOSHI:-MMadereva wanapoficha Magari na Kuanza kucheza Mpira Stendi…..’’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, March 24, 2014

MGOMO WA MADEREVA MOSHI:-MMadereva wanapoficha Magari na Kuanza kucheza Mpira Stendi…..’’


Kutokana na mgomo huo ndipo madereva wa magari hayo na makondakta wakaamua kugeuza stendi hiyo uwanja wa mpira wa miguu likapigwa soka kati ya madereva na makondakta.


Kituo kikuu cha mabasi yaendayo sehemu mbalimbali ndani ya mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ikiwa haina gari baada ya wamiliki wa magari yaendyo maeneo hayo kugoma kutoa huduma leo March 24,2014..

Ndipo askari walipoamua kuingilia kati na kuzuia mchezo huo uliokuwa hauna waamuzi wala milingoti ya kufunga magoli.

Aidha Wakazi wa mji wa Moshi ,Mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania wamepatwa na adha kubwa ya usafiri kuanzia asubuhi ya leo  march 24,2014, kufuatia mgomo huo wa madereva wa daladala na mabasi yaendayo Arusha kupinga faini kubwa zinazotozwa na trafiki.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama amelazimika kuingilia kati suala hilo na kufanya mkutano na wadau katika kuhakikisha kuwa hali ya usafiri inarejea kama kawaida.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad