Tazama Picha za matukio ya Bunge Maalum la Katiba likimemchagua Bi.Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, March 14, 2014

Tazama Picha za matukio ya Bunge Maalum la Katiba likimemchagua Bi.Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo.


Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samia Suluhu Hassan akimkumbatia Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta jana March 13,2014,Mjini Dodoma…Picha na Hassan Silayo MAELEZO.

Mgombea wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la katiba Bi. Amina Abdallah akimpongeza Bi. Samia Suluhu Hassan baada ya Kutangazwa kuwa Makamu mweyekiti wa Bunge Maalum la Katiba.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Samia Suluhu Hassan akitoa shukrani zake kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba baada ya Kuteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mwenyekiti Mteule wa Bunge hilo Bw. Samwel Sitta akibadilishana Mawazo na Mjumbe wa Bunge Hilo Mohamed Seif Khatib ndani ya Ukumbi wa Bunge Jana March 13,2014, Mjini Dodoma.

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashilila akieleza wajumbe juu ya utaratibu wa upigaji kura kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti jana Mjini Dodoma.

Mgombea wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la katiba Bi. Amina Abdallah akinadi Sera zake  kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.

Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba wakibadilishana Mawazo na Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta(Aliyekaa).

Aidha Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wamemchagua Bi.Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo.

Katika uchaguzi huo umefanyika Jana March 13,2014, jioni katika ukumbi wa Bunge hilo Mjini Dodoma, Bi.Suluhu ambaye ni Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, alikuwa akichuana na Bi Amina Abdallah Amour ambaye ni Mbunge wa viti maalum kupitia CUF.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi, Mwenyekiti wa uchaguzi huo, amesema Bi.Suluhu amepata kura 390 sawa na asilimia 74.6, ambapo Bi .Amour amepata kura 126 ambazo ni sawa na asilimia 24.1.

Aidha Leo March 14,2014, asubuhi Katibu na Naibu Katibu wa Bunge hilo wataapishwa kabla ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kuapishwa jioni pamoja na wajumbe wa Bunge hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad