Taswira ya Ushirikina huu njia Panda ni balaaaa.......SOMA. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, March 10, 2014

Taswira ya Ushirikina huu njia Panda ni balaaaa.......SOMA.


Kwa mujibu wa Wikipedia,Ushirikina ni wazo ambalo halina sababu yenye msingi katika maarifa, au mang'amuzi.

Neno hili hutumiwa kwa kutaja imani ambazo hazina msingi. Hii inasababisha baadhi ya ushirikina kuitwa "Hadithi za kale za wake". Pia kwa kawaida hutumiwa katika imani na mazoea zinazohusu bahati au utabiri ambapo matukio ya baadaye yanabashiriwa na matukio yasiyohusiana.

Na kwa mujibu wa mtandao wa islamtanzania.org:-Unaelezea kuwa,USHIRIKINA wa matambiko unatokana na imani kuwa mababu waliofariki wana uwezo wa kuona matendo ya watoto na wajukuu wao walio hai. 

Na inadhaniwa wanapokasirika basi watoto hupata matatizo ya magonjwa, vifo au mabalaa mengine. Na ili kupoza hasira zao huko "walikolala" basi hupikwa mapombe na vyakula vinavyokwenda kumwagwa makaburini au kuliwa na waganga.
 
Katika baadhi ya makabila hata viapo huwa ni kuwataja mababu moja kwa moja au kwa ishara, "alikolala tena!", nikamfufue!, yaani huyo anayesema anathibitisha akimshuhudisha babu au baba yake aliyekufa kuwa akisemacho ni sahihi! 

Ushirikina wa matambiko huandamana na mihanga ya pombe au vyakula ili kuilaza mizimu "iliyochachamalia" koo, familia au jamii fulani. 

Mpaka hii leo bado wako watu wenye imani hizo potofu za kishirikina ambazo huwafanya wasiweze kuendesha mambo yao kwa namna inayotakikana kwa hofu ya kuwachukiza mabab.

Kila kabila lina aina ya matambiko linayofanya kulingana na mila zake. Makabila ya maeneo ya pwani na morogoro hufanya matambiko yao makaburini na kupeana majina maalum ya mababu na kuvaa kago (alama) mikononi. 

Makabila mengine hasa ya mikoa ya kaskazini, kati na magharibi hushikamana na mila au desturi zao za mavazi, ngoma za mashetani, mizuka na vinyamkera vyao kama alama ya kuwaheshimu na kuwaenzi mababu zao wa kale. 

Kwa mfano wamanyema wana ngoma za mizuka, katika ngoma hizo hupandishwa mashetani kulingana na tawi husika la kabila hilo kubwa nchini. Yapo mashetani ya kiluwa, kitongo, kisonge, kibangubangu, kibwari, kibisa nakadhalika. 

Wamakonde nao wanaitakidi kuwa kinachitwadi ndio wanaoua watu kwa hiyo wanadhani kwa kumdanganya kuwa aliyekufa ndiye mtu wa mwisho wanadhani wanaweza kukiepuka kifo! Desturi hii hutumika wakati wa kwenda kuzika! 

Wanyamwezi nao wana mashetani yao ya kike na kiume, wamwelu ni shetani la kike huitwa kwa kupigiwa ngoma inayoitwa migabho, waliopandisha mizuka hiyo hufyonza damu ya mbuzi aliye hai. Baadhi ya vyakula huwa "mwiko kabisa" kwa wenye mashetani hayo. 

Wapo Waswezi nao kama wanyamwezi mwenendo ni huo huo. 

Kauli ya Qur'an dhidi ya imani hizi za kishirikina ni kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa kwani Yeye ndiye aliyewaumba watu wote waliotangulia na waliopo hivi sasa na ndiye pekee aliyewafisha wote waliotangulia. 

Watu wanakatazwa wasiabudie mababu, mizimu wala mizuka kwa matambiko na mihanga, poza na mengineyo bali wanatakiwa wamuabudie:-

"Mola wa mbingu na Ardhi na vilivyomo ndani yake, ikiwa mnayo yakini. Hakuna aabudiwaye kwa haki ila yeye, anahuisha na kufisha, Mola wenu ni Mola wa Wazee wa mwanzo(44:8). 

Eny watu! Mwabuduni Mola wenu ambaye amekuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu ili mpate kuokoka. Ambaye amekufanyieni hii ardhi kuwa kama busati na mbingu kuwa kama paa, na akateremsha maji kutoka mawinguni na kwa hayo akatoa matunda yawe riziki zenu. Basi msimfanyie Allah washirika na hali nyinyi mnajua(2:21-22).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad