LIGI YA MAKOYE 2014:-Cheki taswira ya Benaco FC walivyopambana na Bodaboda FC katika uwanja wa Benaco wilayani Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, March 11, 2014

LIGI YA MAKOYE 2014:-Cheki taswira ya Benaco FC walivyopambana na Bodaboda FC katika uwanja wa Benaco wilayani Ngara mkoani Kagera.

Kikosi cha timu ya Benaco FC kilichoifunga Bodaboda FC bao 1-0 katika mchezo wa Ligi ya Makoye,ikishirikisha timu 8 kutoka kata ya Kasulo,wilayani Ngara mkoani Kagera ,Ligi hiyo ilianza March 01,2014,hadi sasa na inachezwa katika uwanja wa Benaco.

Kikosi cha timu ya Bodaboda FC wapinzani wa Jadi wa Benaco FC kikipiga picha kabla ya kuanza mchezo wake dhidi ya Benaco FC(March 09,2014) Bodaboda FC katika mchezo huo ilifungwa bao 1-0 na Benaco FC.
Mchezo ukiendelea katika uwanja wa Benaco,kata ya Kasulo wilayani Ngara.
Diwani wa kata ya Kasulo,Mh.Philibert Kiiza mwenye shati la pinki akifatilia mchezo huo wa Ligi ya Makoye 2014,kati ya Benaco FC  dhidi ya Bodaboda FC katika kuwania zawadi ya Ngombe -Mnyama.
Mdhamini wa Ligi ya Makoye 2014 kwa kata ya Kasulo,Othumani Makoye (katikati) akifatilia mchezo wakti ya Benaco FC v/s Bodaboda FC katika uwanja wa Benaco na ameahidi kutatua baadhi ya changamoto ya vifaa vya michezo kwa timu 8 zinazoshiriki Ligi hiyo ili zishiriki ipasavyo.
Aliekanyaga mpira ni Mwenyekiti wa Mashindano hayo ya Makoye,Braitoni Kemikimba na Mratibu wake Nuru Buchwa(kulia wakifatilia moja kati ya mechi za Ligi ya Makoye katika uwanja wa Benaco.
Kikosi cha timu ya Bodaboda  FC kikijadiliana namna ya kucheza na kuwakabili wapinzani wao Benaco FC ambapo katika mchezo huo Bodaboda FC walifungwa bao 1-0.
Kikosi cha timu ya Benaco FC kilichoifunga Bodaboda FC bao 1-0 katika mchezo wa Ligi ya Makoye,kikiwa katika Mapumziko ya kipindi cha kwanza ya mchezo wake na Bodaboda FC.
Mashabiki wa timu hizo Bodaboda FC na  Benaco FC wakifatilia mchezo huo uliochezwa  March 09,2014, katika  uwanja wa Benaco.
Mashabiki wa timu hizo Bodaboda FC na  Benaco FC wakifatilia mchezo huo uliochezwa  March 09,2014, katika  uwanja wa Benaco.


Ligi hiyo ya Makoye 2014,inashirikisha timu 8 kutoka kata ya Kasulo pekee zilizopangwa katika kundi A lenye timu za Kumunazi Star,Nguvu Kazi FC,Rusumo Sekondari na Kisabule FC huku kundi  B likiwa na timu za Watumishi Shooting Star,Benaco Star,Kago Star na Bodaboda FC ambapo kila kundi litatoa timu mbili zitakazoingia hatua ya nusu fainali.

Nuru Buchwa ambaye ni mratibu wa Ligi ya Makoye 2014,amebainisha kuwa Bingwa wa Ligi hiyo ataondoka na zawadi ya Ng’ombe mwenye thamani ya shilingi Laki 3,Mshindi wa pili fedha taslimu shilingi 100,000/=,watatu shilingi Elfu 50 ,pamoja na Mchezaji bora na mfungaji bora kuondoka na shilingi Elfu 10 na Timu yenye nidhamu itaondoka na Kreti moja la soda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad