Mbunge wa
jimbo la Iringa mjini Mh.PETER MSIGWA kwa mara nyingine
amefikishwa leo katika mahakama kuu ya mkoa , kufuatia
tuhuma inayomkabili ya kufanya vurugu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa
udiwani katika kata ya nduli manispaa ya iringa.
Tukio hilo
limetoke tarehe 6 ya mwezi wa pili ambapo SALUM KEITA mjumbe
wa kampeni hizo kupitia chama cha mapinduzi alidai kufanyiwa
vurugu na mbunge wa jimbo la iringa mjini kwa kumpiga.
Kesi hiyo
imesomwa leo katika mahakama ya wilaya ya Iringa mbele ya
jaji ALOYCE MASUA na kesi hiyo
imeahirishwa na kutajwa kusikilizwa tarehe 9 ya mwezi wa 4 mwaka huu.





No comments:
Post a Comment