![]() |
|
Mkuu wa Kikosi
cha Usalama Barabarani Chalinze mkoani Pwani, Innocent Sull akiangalia lori la
mafuta lililogongana na basi dogo eneo la Bwawani na kusababisha kifo cha mtu
mmoja.
|
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine
14 kujeruhiwa baada ya basi dogo kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la
Bwawani katika Barabara ya Chalinze - Morogoro.
Ajali hiyo ilitokea jana (March 06,2014) saa 4.30 asubuhi
baada ya basi hilo aina ya Toyota Coaster lililokuwa likitokea Dar es Salaam
kwenda Ifakara kugongana na lori la mafuta lililokuwa likitoka Morogoro
kuelekea Chalinze.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,
Ulrich Matei alimtaja aliyefariki dunia katika ajali hiyo ni dereva wa lori,
Ally Ngoma (62).
Kamanda Matei alisema majeruhi 14 wa
ajali hiyo ni abiria waliokuwa kwenye basi. Alisema wote walipelekwa katika
Kituo cha Afya Chalinze kwa matibabu.
Alisema ajali hiyo ilitokea baada ya
dereva wa basi kujaribu kuyapita magari mengine katika eneo la Sekondari ya
Bwawani sehemu ambayo ina mwinuko.
Alisema wakati dereva huyo akijaribu
kuyapita magari hayo, alikutana na lori hilo na kugongana uso kwa uso na
kusababisha kifo na majeruhi hao.
Alisema dereva wa basi hilo
anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa kujibu tuhuma
zinazomkabili.
Mbali ya kusababisha kifo na
majeruhi hao, ajali hiyo ilisababisha adha kwa waliokuwa wakitumia barabara
hiyo hasa wale wanaosafiri kati ya Dar es Salaam na Morogoro kwani zaidi ya
magari 200 yalikwama kwa zaidi ya saa tatu.
Ajali hiyo imetokea siku moja baada
ya nyingine iliyosababisha vifo vya watu saba baada ya basi dogo la abiria
kugongana na lori katika eneo la Chalinze Mzee na kujeruhi tisa.
Akizungumzia ajali hiyo ya juzi,
Ofisa Habari wa Hospitali ya Tumbi, Kibaha, Gerald Chami alisema majeruhi sita
hali yao wanaendelea vyema.






No comments:
Post a Comment