![]() |
|
Jumla ya
Walimu wapya 36,021 ambao wamehitimu mwaka 2013 kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini
Tanzania wataajiriwa rasmi na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri)
ifikapo tarehe 01 Aprili 2014.
|
Kati ya
idadi hiyo walimu wa ngazi ya Cheti (Daraja III A) ambao hufundisha katika
shule za Msingi ni 17,928 na walimu wa shule za sekondari ni 18,093 (wakiwemo
5,416 wa Stashahada na 12,677 wenye shahada.
Orodha rasmi
ya walimu wapya ikionesha Halmashauri mbalimbali walikopangwa itatangazwa
kwenye tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI www.pmoralg.go.tz na
ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi www.moe.go.tz ifikapo tarehe
15 Machi, 2014.
Walimu wote
wapya wanatakiwa kuripoti bila kukosa kwenye Halmashauri walikopangiwa ifikapo
tarehe 01 Aprili, 2014 ili waanze kazi mara moja.
Inasisitizwa
kwamba walimu waripoti tarehe hiyo ili taarifa zao za kiutumishi zifanyiwe kazi
na Waajiri wao yaani Wakurugenzi ili kuwawezesha kupata mshahara mwezi Aprili
2014 na hivyo kuepuka ulimbikizaji wa mshahara kwa watumishi wapya wanaoanza
ajira.
Mwalimu
yoyote ambaye ataripoti baada ya tarehe 10 Aprili, 2014 bila sababu za msingi zinazokubalika
kiutumishi atakuwa amepoteza nafasi hiyo.
Ikumbukwe
kwamba Upangaji wa Walimu wapya kwenye Halmashauri umezingatia uwepo wa mahitaji
ya walimu Vile vile, fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba na nauli ambazo
zitalipwa kwa kila mwalimu atakayeripoti kulingana na viwango vilivyowekwa na
Serikali zimetumwa kwenye Halmashauri walikopangwa
walimu hao Hivyo,kila mwalimu anatakiwa kwenda kuripoti katika Halmashauri
alikopangwa.
Ofisi ya
Waziri Mkuu TAMISEMI haitafanya mabadiliko yoyote ya vituo vya kufanya kazi
walimu wapya isipokuwa kwa utaratibu wa kawaida wa uhamisho baada ya mwalimu
kutimiza vigezo na masharti ya hamisho.
Ni vema
ifahamike kuwa ajira zinazotangazwa ni za walimu wapya Walimu ambao tayari ni
watumishi umma waliokuwa vyuoni kwa ajili ya kujiendeleza kielimu na hivi sasa
wamehitimu mafunzo yao, wanatakiwa
kurudi kwa waajiri wao na kuendelea na kazi.
Imetolewa na:-
Jumanne A.Sagin
Katibu
Mkuu
TAMISEMI






No comments:
Post a Comment