Serikali yatoa Milioni 150 ,kwa wilaya ya Ngara mkoani Kagera kwa ajili ya kuboresha na kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma ya maji safi na salama. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, March 22, 2014

Serikali yatoa Milioni 150 ,kwa wilaya ya Ngara mkoani Kagera kwa ajili ya kuboresha na kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma ya maji safi na salama.


Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanal Mstaafu Fabian Masawe(kushoto) anaekunywa maji safi na salama,aliyefanya ziara ya kutembelea miradi ya maji  wilayani Ngara ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Maji…pembeni yake ni Mkuu wa wilaya ya Ngara, Bw Constantine Kanyasu(aliyesimama).


Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania imetoa Sh bilioni 8.2 ,kwa mkoa wa Kagera kwa ajili ya kuboresha na kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma ya maji safi na salama ya uhakika hasa Vijijini ifikapo mwaka 2015.
Serikali imetoa Sh milioni 150 , kwa wilaya Ngara mkoani Kagera kwa ajili ya kuboresha mradi wa maji mjini Ngara ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa mwaka jana alipofanya ziara wilayani Ngara.

Mkuu wa wilaya ya Ngara, Bw Constantine Kanyasu amebainisha hayao March 20,2014, wakati akisoma taarifa ya wilaya  hiyo ,kwa mkuu wa mkoa wa Kagera Kanal Mstaafu Fabian Masawe aliyefanya ziara ya kutembelea miradi ya maji  wilayani humo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Maji.

Bw Kanyasu amesema kuwa Rais  ametuma fedha  hizo ili   kuboresha na kupanua mradi wa maji mjini Ngara na kwamba  fedha hizo zitatumika kwa kununua mtambo mpya wa kusukuma maji utakaofungwa katika kisima kipya kilichochimbwa pamoja na kuongeza vyanzo vya maji kutoka visima viwili virefu hadi kufika visima vitatu .

Bw Kanyasu amewataka wataalam katika Mamlaka ya Maji na viongozi wengine kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuondokana na malalamiko ya wananchi kuhusu huduma ya maji isiyokidhi mahitaji na Kuongeza uzalishaji wa maji kutoka kiwango cha sasa cha 76%.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad