Mbeya City nafasi ya Pili,waivuta Yanga SC hadi nafasi ya 3 baada ya kuichapa Rhino Rangers ya Tabora Bao 3-1. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, March 09, 2014

Mbeya City nafasi ya Pili,waivuta Yanga SC hadi nafasi ya 3 baada ya kuichapa Rhino Rangers ya Tabora Bao 3-1.



Wagonga nyundo wa Mbeya, klabu ya Mbeya City wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya maafande wa Rhino Rangers katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara ndani ya dimba lao la Sokoine jijini Mbeya  Jana March 08,2014.

Ligi Kuu Vodacom, iliendelea Leo March 08,2014 na huko Uwanja wa Sokoine, Jijini Mbeya, Wana wa Nyumbani, Mbeya City, wameicharaza Rhino Rangers ya Tabora Bao 3-1 na kukamata Nafasi ya Pili na kuwashusha Mabingwa Watetezi Yanga toka Nafasi hiyo.

Mbeya City sasa wamecheza Mechi 21 na wana Pointi 39 wakiwa Pointi 1 moja mbele ya Yanga SC, ambao wamecheza Mechi 17 tu, na Pointi 1 nyuma ya Vinara Azam FC waliocheza Mechi 18.

Huko Mkwakwani, Tanga, Wenyeji Coastal Union walitoka 0-0 na Ashanti United na huko Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Mkoani Pwani, Ruvu Shooting iliitungua JKT Oljoro Bao 1-0 kwa Bao la Ayub Kitala.

Ligi itaendelea Jumapili kwa Mechi mbili huko Mbeya na Dar es Salaam ambako Uwanja wa Sokoine, Mbeya, utakuwa na Mechi ya Tanzani Prisons na Simba SC na huko Azam Complex, Chamazi, Viunga vya Dar es Salaam, JKT Ruvu watacheza na Mtibwa Sugar.

LIGI KUU VODACOM TANZANIA BARA 2013/2014.

Jumapili Machi 9,2014.

Tanzania Prisons v Simba
JKT Ruvu v Mtibwa Sugar

MATOKEO.

Jumamosi Machi 8,2014.

Coastal Union 0 Ashanti United 0
Mbeya City 3 Rhino Rangers 1
Ruvu Shooting 1 JKT Oljoro 0


MSIMAMO.

NA TIMU P W D L GD PTS
1 Azam FC 18 11 7 0 23 40
2 Mbeya City 21 10 9 2 10 39
3 Yanga SC 17 11 5 1 29 38
4 Simba SC 20 9 8 3 17 35
5 Kagera Sugar 20 7 8 5 2 29
6 Ruvu Shooting 20 7 7 6 -4 28
7 Coastal Union 20 5 11 4 5 26
8 Mtibwa Sugar 19 6 7 6 0 25
9 JKT Ruvu 20 7 1 12 -14 22
10 Prisons FC 18 3 9 6 -3 18
11 Mgambo JKT 20 4 6 10 -17 18
12 Ashanti United 21 4 6 11 -18 18
13 JKT Oljoro 21 2 9 10 -16 15
14 Rhino Rangers 21 2 7 12 -14 13

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad