Chelsea sasa point 7 kileleni mwa Ligi Kuu ya England huku Manchester United ikiwapa faraja mashabiki wake kwa kuitandika mabao 3-0 West Brom. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, March 09, 2014

Chelsea sasa point 7 kileleni mwa Ligi Kuu ya England huku Manchester United ikiwapa faraja mashabiki wake kwa kuitandika mabao 3-0 West Brom.



Mimi kizee; Eto'o akishangilia kama mzee baada ya kufunga kuwabeza wanaomuita mzee kwenye timu hiyo, baada ya kocha Jose Mourinho pia kusema ana umri mkubwa, Ushindi huo, unaifanya Chelsea itimize pointi 69 baada ya kucheza mechi 28 na kujiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu Uingereza , ikiizidi kwa pointi saba Liverpool iliyo nafasi ya pili kwa pointi zake 59 sawa na Asrenal, nao wakiwa wamecheza mechi 28 pia. Manchester City ni ya nne sasa kwa pointi zake 57, lakini ina mechi mbili mkononi.
Chelsea wamejichimbia kileleni mwa Ligi Kuu England kwa kuichapa Tottenham Bao 4-0 na kuongoza Ligi wakiwa Pointi 7 mbele.

Hadi Mapumziko Mechi hii ilikuwa 0-0.

Kipindi cha Pili, makosa ya Jan Vertonghen yaliwafungulia Chelsea mvua ya Magoli baada ya kuteleza akiwa na Mpira na katika jitihada za kuokoa akatoa pasi kwa Samuel Eto’o ambae alifunga na kusherehekea kama Mtu Mzee ikiwa ni ishara ya kumkejeli Meneja wake Jose Mourinho ambae Wiki iliyopita alirekodiwa akisema hajui Umri wa Eto’o na hilo kuibua utata kuhusu Umri wa Straika huyo toka Cameroun.

Bao hilo lilidumu Dakika 5 tu na kwenye Dkika ya 60 Tottenham walipata mapigo mawili baada Refa Michael Oliver kuwapa Penati Chelsea na pia kumpa Kadi Nyekundu Sentahafu wao Younes Kaboul kwa kumchezea Rafu Samuel Eto’o.

Eden Hazard alifunga Penati hiyo na Chelsea kuongoza 2-0.

Chelsea waliongeza Bao nyingine, zote kupitia Demba Ba alieingizwa badala ya Eto’o katika Dakika ya 76, na zote zilitokana na makosa ya Mabeki wa Tottenham huku moja likifungwa baada Sandro kuteleza na jingine Kichwa cha Kyle Walker kunaswa kabla kumfikia Kipa Hugo Lloris.


Wayne Rooney akishangilia bao lake aliloifungia Manchester United dhidi ya West Brom Jana March 08,2014,pale Manchester United ikiwapa faraja mashabiki wake baada ya kikosi hicho cha David Moyes kuitandika mabao 3-0 West Brom.

Mabingwa watetezi wa Uingereza, Manchester United, wakicheza Ugenini huko The Hawthorns, wameichapa West Bromwich Albion Bao 3-0 na kupanda Nafasi moja na kukamata Nafasi ya 6.


Bao la Kwanza la Man United lilifungwa kwa Kichwa na Phil Jones katika Dakika ya 34 kufuatia Frikiki ya Robin van Persie.

Man United walifunga Bao la Pili kupitia Wayne Rooney kwa Kichwa katika Dakika ya 65 alipounganisha Krosi ya Rafael baada muvu aliyoanzisha mwenyewe na kumhusisha Juan Mata aliempa Rafael.

Bao la Tatu lilifungwa na Danny Welbeck baada ya gonga safi ya Pasi 7 zilizomfikia Rooney aliempenyezea Welbeck na kufunga katika Dakika ya 82.

Mechi inayofuata kwa Man United ni Jumapili Machi 16 Uwanjani Old Trafford watakapocheza na Mahasimu wao wa Jadi, Liverpool.

LIGI KUU ENGLAND:-MATOKEO.
 
Jumamosi Machi 8,2014.
West Brom 0 Man United 3
Cardiff 3 Fulham 1
Crystal Palace 0 Southampton 1
Norwich 1 Stoke 1
Chelsea 4 Tottenham 0
MSIMAMO.

NA TIMU P GD PTS
1 Chelsea 29 34 66
2 Liverpool 28 38 59
3 Arsenal 28 24 59
4 Man City 26 42 57
5 Tottenham 29 0 53
6 Man United 28 12 48
7 Everton 27 11 48
8 Newcastle 28 -2 43
9 Southampton 30 2 42
10 West Ham 28 -4 31
11 Aston Villa 28 -7 31
12 Stoke 29 -14 31
13 Hull 28 -5 30
14 Swansea 28 -4 29
15 Norwich 29 -22 29
16 Crystal Palace 28 -19 27
17 West Brom 28 -11 25
19 Cardiff 29 -28 25
18 Sunderland 26 -16 24
20 Fulham 29 -36 21


MECHI ZIJAZO LIGI KUU.

Jumamosi Machi 15,2014.

1545 Hull v Man City
1800 Everton v Cardiff
1800 Fulham v Newcastle
1800 Southampton v Norwich
1800 Stoke v West Ham
1800 Sunderland v Crystal Palace
1800 Swansea v West Brom
2030 Aston Villa v Chelsea

Jumapili Machi 16,2014.

1630 Man United v Liverpool
1900 Tottenham v Arsenal

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad