HABARI:- Mkuu wa Mkoa wa Kagera agiza Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Ngara, kuzikatia huduma ya maji taasisi za serikali zinazodaiwa zaidi ya Sh milioni 8. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, March 20, 2014

HABARI:- Mkuu wa Mkoa wa Kagera agiza Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Ngara, kuzikatia huduma ya maji taasisi za serikali zinazodaiwa zaidi ya Sh milioni 8.



Muonekano wa Mto Ruvubu/Ruvuvu ukianzia nchini Burundi na kupita wilayani Ngara mkoani Kagera na kutengeneza maporomoko ya Rusumo(mpakani mwa Tanzania na Rwanda-Daraja la rusumo)pamoja na changamoto mbalimbali za kubaki kuwa moja ya Hustoria ,ila umekuwa ni moja wa Chanzo cha Maji japo si safi na salama kwa baadhi ya wakazi mto huo unapopita.


 Mto Ruvubu/Ruvuvu ukionekana ambapo hukutana na maji ya Mto Kagera na kutengeneza maporomoko ya Rusumo.


Maporomoko ya Rusumo yakipatikana  wilayani Ngara mkoani Kagera mpakani mwa Tanzania na Rwanda-Daraja la rusumo).


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe ameiagiza Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira wilayani Ngara mkoani humo, kuanza kuzikatia huduma ya maji taasisi za serikali zinazodaiwa zaidi ya Sh milioni 8 na laki 3.

Kanali Massawe ametoa agizo hilo leo March 20,2014, wilayani Ngara, muda mfupi baada ya kusomewa taarifa ya wilaya hiyo, kuhusu maadhimisho ya wiki ya maji, iliyosomwa na Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Constantine Kanyasu.

Amesema serikali haitazivumilia taasisi zake zinazolimbikiza Ankara za maji, hali inayosababisha kukwama kwa utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi.

Akisoma taarifa ya wilaya, Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Costantine Kanyasu amesema kuwa taasisi za Magereza na Polisi, hadi kufikia mwezi Februari mwaka huu zilikuwa zinadaiwa zaidi ya Sh milioni 8 na laki 3 hali inayosababisha kukwama kwa shughuli za usambazaji maji.

Habari Na:-Radio Kwizera FM.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad