Hapo Juzi tarehe 18/03/2014 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
nchini Jaji Joseph Sinde Warioba aliwasilisha kwenye Bunge maalum la Katiba rasimu
ya pili ya katiba.
Kwasababu ya maombi hayo CCM imeona bora kueleza kwa mara nyingine tena
msimamo na imani ya CCM juu ya swala zima la Muungano na muundo wake.
Kimsingi CCM ndio waasisi wa Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar. CCM
inamasilahi makubwa na mapana na Muungano huu kama waasisi pengine kuliko
taasisi nyingi ndani na nje ya nchi yetu.
Bado CCM inaamini changamoto za Muungano huu suluhisho lake sio kubadili
muundo wa Muungano bali ni kuufanyia maboresho muundo wa muungano tulionao wa
serikali mbili. Hivyo basi CCM bado inaamini muundo bora kwasasa utakao dumisha
muungano wetu ni muundo wa SERIKALI MBILI.
Kwakuwa kazi ya Warioba na Tume yake sasa imekwisha rasmi, kuisha kwa
kazi yao ni mwanzo wa awamu nyingine ya mchakato huu. Mwisho wa kazi ya Tume
sio mwisho wa mjadala juu ya Katiba tuitakayo bali ni mwanzo wa awamu nyingine
ya mjadala mpana na maboresho kama sio marekebisho ya kuondoa mapungufu kwenye
rasimu iliyowasilishwa.
Mwanzo wa awamu hii nyingine ni furusa nzuri ya kupima kama kweli
yaliyomo kwenye rasimu na maelezo ya ziada yaliyotolewa na Jaji Warioba yana
akisi maoni ya Watanzania walio wengi.
CCM ina amini awamu mbili zilizobaki kwakuwa zinahusisha
wawakilishi wa wananchi kupitia Bunge maalum la Katiba, na hatimaye
itawahusisha wananchi wenyewe moja kwa moja kupitia kura yao, zitatumika vizuri
kutupa ni nini hasa matakwa ya Watanzania juu ya Katiba waitakayo na sio maoni
au matakwa ya wachache.
Wakati haya yote yakiendelea CCM bado tunaamini Muungano huu ni muhimu
ukadumishwa na kuimarishwa. CCM tunaaamini ili Muungano huu udumu njia pekee
kwasasa ni kufanya marekebisho kwenye Muundo wa serikali mbili ili ujibu vizuri
zaidi changamoto mbalimbali zilizoibuliwa na kukidhi mazingira ya sasa.
Tunawaomba wanaCCM na watanzania kwa ujumla kuwa watulivu katika kipindi
hiki. Ni vizuri Watanzania tukavumiliana,tukashindana kwa hoja tukitanguliza
mbele uzalendo na masilahi ya kweli ya nchi yetu.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na;-
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
20/03/2014







No comments:
Post a Comment