Katibu
tawala wa mkoa wa Mara, Bw Benedict Ole Kuyan, amesema kuwa Bw. Tuppa kabla ya
kifo chake leo asubuhi akiwa na afya njema alifika katika ofisi za mkoa na
kumuaga kuwa anakwenda kufunga mafunzo ya mgambo katika kijiji cha Nyamwaga
wilayani Tarime.
Amesema kuwa muda mfupi baada ya kufika katika ofisi ya mkuu wa wilaya, alipatwa na tatizo la ugonjwa huo na muda mfupi alikimbizwa hospitali ya Tarime lakini alifariki wakati akipatiwa matibabu.
Katibu tawala huyo amesema mwili wa marehemu unasafarishwa kutoka Tarime kuja hospitali ya Musoma kwa ajili ya kuhifadhiwa wakati taratibu nyingine na maelekezo ya kiserikali yakisubiriwa kutolewa.

No comments:
Post a Comment