Hili ndilo Shimo Lililosababisha Ajanali ya basi la Zuberi likitoka Ngara kwenda Mwanza eneo la Nyabugombe na Kujeruhi mtu Mmoja. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, March 26, 2014

Hili ndilo Shimo Lililosababisha Ajanali ya basi la Zuberi likitoka Ngara kwenda Mwanza eneo la Nyabugombe na Kujeruhi mtu Mmoja.

Ni muonekano wa mashimo katika Barabara ya Nyakanazi-Ngara eneo la mteremko mkali wa Nyabugombe mpakani mwa Wilaya ya Ngara na Biharamulo mkoani Kagera,ambalo inaelezwa ndilo chanzo cha Ajali ya Basi la Zuberi iliyotokea Jana March 25,2014,Asubuhi katika eneo hilo na kujeruhi Abiria mmoja ambae alivunjika mkono na kulazwa katika Hospitali ya Murgwanza wilayani Ngara.

Shimo hili ndilo lilisababisha kukwama kwa Lori la Mizigo upande wa kushoto wa Barabara hiyo ya Nyakanazi-Ngara wakatilikipanda mlima huo wa Nyabugombe ambapo basi la Zuberi lilipofika eneo hilo lilivaa shimo hilo hali iliyosababisha Meni Livu na Sekandi Livu kukatika  hivyo gari kuhama njia na kupinduka kama baadhi ya Picha chini zikionesha.






Kutokana na ubovu wa barabra hiyo baadhi ya magari makubwa ya mizigo yanayopita yamekuwa yakikwama kwa kushindwa kupanda  mlima vyema hali inayosababisha wakati mwingine foleni.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad