![]() |
|
Mabao hayo
yalifungwa na Ngassa dakika ya 14 na Cannavaro dakika ya 20, wote wakitikisa
nyavu kwa kichwa baada ya mipira kutoka pembeni.
|
Yanga SC
imetanguliza mguu mmoja Raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kufuatia
ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Komorozine ya Comoro jioni hii katika mchezo wa
kwanza wa Raundi ya Awali, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Washambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa alifunga mabao matatu, Mrundi Didier Kavumbangu mawili, Mganda Hamisi Kiiza moja na lingine beki Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’.
Kwa ushindi huo, Yanga sasa inahitaji sare au kufungwa si zaidi ya mabao 6-0 katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo ugenini ili kusonga mbele, ambako itakutana na Al Ahly ya Misri.
Nayo Azam
inaikaribisha Ferroviario de Beira ya Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa
raundi ya awali ya CC utakaochezwa Jumapili (Februari 9 mwaka huu) saa 10
kamili kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.






No comments:
Post a Comment