Aidha ratiba hiyo inaonyesha kwamba mshtakiwa akisomewa mashtaka na kujibu, mahakama itapanga tarehe ya kusikiliza maelezo ya awali dhidi ya kesi hiyo.
Mnamo Januari 29, mwaka 2013 Lulu aliachiwa kwa dhamana baada ya
kesi hiyo kubadilishwa hati ya mashitaka kutoka kwenye kesi ya mauaji kwenda
mauaji ya bila kukusudia.
Aidha, Lulu alipata dhamana hiyo baada ya Jaji Zainabu Mruke kutoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa huyo baada ya wakili wa utetezi Peter Kibatala kuwasilisha maombi ya dhamana kwa hati ya dharula chini ya kifungu cha 148 kidogo cha (1) na cha (2) cha Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA). Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Joseph Maugo na Kishenyi Mutalemwa.
Wakili Kibatala alidai kuwa hati hiyo
imeambatanishwa na hati ya mashtaka yanayomkabili Lulu la kuua bila kukusudia
na kwamba kwa mujibu wa shtaka hilo mshtakiwa ana haki ya kupata dhamana.
Upande wa Jamhuri, ulidai kuwa hauna
pingamizi la maombi hayo na kwamba mahakama ijielekeze kwenye kifungu cha 148
kidogo cha (6)ambacho kinamtaka mshtakiwa kufuata masharti yatakayotolewa chini
ya kifungu hicho.
Jaji Mruke alisema kosa linalomkabili
mshakiwa lina dhamana kisheria na kwamba mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa
kufuata masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali
watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. milioni 20 kila mmoja.
"Tukubaliane wote kwamba hakuna ubishi
roho ya mtu imepotea hivyo sheria lazima ifuatwe... pia mshtakiwa awasilishe
hati zake za kusafiria, kuripoti kila tarehe Mosi ya mwezi kwa Msajili wa
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, asitoke nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila
kibali cha msajili huyo" alisema Jaji Mruke.
Alisema Msajili wa Kanda ya Dar es
Salaam ahakiki masharti ya dhamana kabla ya mshtakiwa hajaachiwa kwa
dhamana. Katika kesi ya msingi, Lulu anadaiwa kuwa Aprili 7, mwaka Sinza
Vatican, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alimuua Kanumba bila kukusudia.


.jpg)



No comments:
Post a Comment