![]() |
Shirika la Misaada kwa watoto, Save the Children, linasema kuwa watoto milioni moja hufariki dunia kila mwaka katika siku yao ya kwanza ya maisha. |
Katika
ripoti mpya ya shirika hilo la misaada kwa watoto linasema vifo vya watoto
wachanga vimesalia kuwa moja ya aibu za dunia ya sasa.
Hali ya
watoto ni mbaya zaidi hasa katika mataifa yanayokabiliwa na mizozo.
Mwandishi wa
BBC aliye Sudan Kusini, Anne Soy, amesema kuwa katika mazingira ya sasa ya
Sudan Kusini, watoto na wanawake, hasa wale wajawazito wanaokabiliwa na athari
nyingi za vita vinavyoendelea nchini humo.
Amesema kuwa
kutokana na vita watoto, walioandamana na wazazi wengine wakiwa pekee,
wanaungana na akina mama kutembelea mwendo mrefu ili kujiepusha na vita vya
kikabila vinavyoendelea nchini.
Miundo
msingi katika Sudan Kusini, kama vile hospitali ni chache sana jambo ambalo
linatatiza maisha ya wanawake na watoto.
Katika
hospitali ya mji wa Nimule kwenye mpaka wa Sudan Kusini na Uganda Kuna vitanda
174 pekee hospitalini idadi ambayo haiafikiana kamwe na maelfu ya wagonjwa na
wahasiriwa wa vita .
Save the
children inasema kuwa vita vinawaathiri zaidi watoto huko Syria, Jamhuri ya
Afrika ya Kati CAR na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Shirika la
Save the Children linasema kuwa vifo hivi vingi vinaweza kuzuiliwa.
Source:-BBC
No comments:
Post a Comment