Hawa ndio washiriki 43 wa Mafunzo ya Ukocha ,Uamuzi na Uongozi katika mchezo wa mpira wa Wavu mkoani Kagera waliokabidhiwa cheti kutoka TAVA. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, February 25, 2014

Hawa ndio washiriki 43 wa Mafunzo ya Ukocha ,Uamuzi na Uongozi katika mchezo wa mpira wa Wavu mkoani Kagera waliokabidhiwa cheti kutoka TAVA.

Picha ya pamoja ya washiriki 43 wa Mafunzo ya siku 7(February 13-19,2014) katika fani ya  ukocha ,uamuzi na uongozi katika mchezo wa mpira wa wavu mkoani Kagera ambapo baada ya kufaulu mtihani walikabidhiwa Vyeti kutoka Chama cha mchezo wa Wavu nchini Tanzania –TAVA.

Baadhi ya washiriki 43 wa Mafunzo hayo ya Ukocha ,Uamuzi na Uongozi katika mchezo wa mpira wa wavu kutoka wilaya 7 za mkoa wa Kagera yaliyofanyika katika ukumbu wa mkuu wa wilaya ya Ngara , yameelezwa na baadhi ya washiriki kuwa yamewasaidia kuelewa sheria mbalimbali zinazotawala  mchezo wa wavu tofauti na hapo mwanzo walivyokuwa hawazijui sheria hizo.
Kushoto ni Mgeni rasmi Cornel Ng'udungi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera,pamoja na mambo mengine aliwataka washiriki hao 43 waliopata cheti kuyatumia mafunzo hayo kuendeleza mchezo wa wavu katika Halmashauri zao mkoani Kagera,kuandaa timu za ushindani,Kuibua vipaji kwa Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari pamoja na kuufanya Mchezo wa wavu mkoani Kagera kuwa chachu ya kuleta maendeleo.kulia kwake ni Afisa Elimu shule za msingi wilaya ya Ngara Saimon Mumbee.
Waliochuchumaa chini ni washiriki wa  Mafunzo hayo ya mpira  wa wavu mkoani Kagera kutoka wilaya ya Ngara mkoani Kagera.
Waliochuchumaa chini ni washiriki wa  Mafunzo hayo ya mpira  wa wavu mkoani Kagera kutoka wilaya ya Kyerwa na Karagwe mkoani Kagera.
Waliochuchumaa chini ni washiriki wa  Mafunzo hayo ya mpira  wa wavu mkoani Kagera kutoka Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera.
Waliochuchumaa chini ni washiriki wa  Mafunzo hayo ya mpira  wa wavu mkoani Kagera kutoka Manispaa ya Bukoba.
Waliochuchumaa chini ni washiriki wa  Mafunzo hayo ya mpira  wa wavu mkoani Kagera kutoka Manyoni mkoani Singida.
Picha ya pamoja kutoka kushoto ni Said Salumu Afisa Michezo wilaya ya Ngara,Samson Mathayo Mwenyekiti wa KAREVA-Chama cha  mchezo wa wavu mkoa wa KAGERA,Afisa Elimu shule za Msingi wilaya ya Ngara ,Saimon Mumbee,Cornel Ng'udungi aliyekuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa mafunzo hayo na pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara, kutoka chama cha cha mchezo wa wavu taifa TAVA-Somo Ahmed Kimwaga,Julius Nestory Afisa Elimu sekondari wilaya ya Ngara na Makamu mwenyekiti wa KAREVA-Dauson Buninange.
Mafunzo hayo ya siku 7(February 13-19,2014) yalikuwa chini ya Mkufunzi ambaye pia ni  Mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya mchezo wa wavu nchini kutoka chama cha cha mchezo wa wavu taifa TAVA-Somo Ahmed Kimwaga(mwenye jezi nyeusi) na alitoa wito kwa Wachezaji wa mchezo wa wavu nchini wametakiwa  kujifunza  sheria zinazotawala  mchezo huo ambazo zimekuwa zikibadilika kila wakati  na kwamba mpaka sasa TAVA imeshatoa elimu ya mchezo huo wa Watanzania 310 katika mikoa 15 nchini(kushoto kwake ni Afisa Michezo na Utamaduni wilaya ya Ngara Salum Bakari .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad