UTAFITI:- Tendo la ndoa; Tiba mbadala ya maradhi ya moyo, ubongo, maumivu ya kichwa? - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, February 10, 2014

UTAFITI:- Tendo la ndoa; Tiba mbadala ya maradhi ya moyo, ubongo, maumivu ya kichwa?


“Kwa mfano, tendo la ndoa linaondoa msongo wa mawazo iwapo unayetenda naye unampenda na  amekupa maandalizi mazuri. Sidhani kama alimradi utende hilo tendo na yeyote litakusaidia,” anasema mtaalamu huyo…Ikumbukwe kuwa utafiti hauchochei watu kufanya mapenzi kiholela, bali unajikita kwa  wanandoa pekee.
Ingawa tendo la ndoa lisipofanywa kwa kuzingatia kanuni na taratibu, sambamba na umakini, linaweza kusababisha maradhi, lakini kwa wanandoa, tendo  hilo linatajwa kuwa na manufaa mengi  kiafya tofauti na faraja ya kawaida iliyozoeleka kwa wengi.

Imefahamika kuwa tendo hili likifanyika ipasavyo husaidia kuondoa msongo wa mawazo, maradhi ya moyo, maumivu ya kichwa yasiyokoma na kupunguza kasi ya saratani ya tezi dume.

 Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (Muhas), Dk Yahya Kishashu anasema inategemea tendo linafanywa na nani na mhusika yupo kwenye mazingira gani.

“Kwa mfano, tendo la ndoa linaondoa msongo wa mawazo iwapo unayetenda naye unampenda na  amekupa maandalizi mazuri. Sidhani kama alimradi utende hilo tendo na yeyote litakusaidia,” anasema mtaalamu huyo.

Anaongeza kuwa  ndiyo maana baadhi ya watu wanatoka nje ya ndoa zao kwa sababu si mara zote tendo la ndoa linawafurahisha wanandoa.

“Wakati mwingine tendo hilo laweza kuwa karaha kwao,” anasema

Mazoezi

Si hivyo tu, utafiti uliofanyika Canada  hivi karibuni umebainisha kuwa kufanya tendo la ndoa kwa kipindi cha dakika 25 kwa wanamume kunachoma kalori 100 na kwa wanawake kalori 69.

Tendo hilo likifanyika kwa nusu saa, linaweza kupunguza kalori za mwili kuliko kutembea kwenye mashine ya mazoezi ya ‘treadmill’.

“Ni sawa na kucheza mpira wa tenisi au kutembea ukipanda mlima kwa dakika 20 au kucheza gofu kwa kasi kwa dakika 33 au zoezi la yoga kwa dakika 40,” sehemu ya utafiti hiyo inasema.

 Utafiti huo wa Canada ulishabihiana na kampeni  iliyofanywa na Taasisi ya Moyo ya Uingereza ambayo ilisema kuwa  dakika 30 za tendo la ndoa kwa siku ni muhimu kama mazoezi ya kutembea kwa mashine.

Kwa undani zaidi utafiti huo ulichambua na kusema kuwa, tendo la ndoa, lina manufaa  kwa moyo na mapafu.

Inaelezwa kuwa vichocheo  vinavyotoka  baada ya tendo la ndoa vinasaidia kupunguza kiwango cha msongo wa mawazo na kuongeza  uzalishaji wa seli mpya za ubongo.

 Kuhusu mazoezi, Dk Kishashu anasema anakubaliana na utafiti huo na kusema kuwa ni kweli tendo hilo linasaidia kupunguza kalori, lakini linapofanyika mara nyingi zaidi linazeesha.

Hata hivyo, wanasayansi wanalipa uzito mdogo tendo hilo katika muktadha wa ujenzi wa hisia na mwili na kuwa halisisitizwi vya kutosha kama aina mojawapo ya mazoezi.

Tiba kwa moyo, mapafu na ubongo

Inaelezwa kuwa tendo la ndoa, linasaidia kuondoa msongo wa mawazo hivyo kupunguza hatari ya maradhi ya moyo.

Si hivyo tu, bali tendo hilo husaidia mapafu kufanya kazi yake vyema, kuingiza na kutoa hewa chafu.

Kitaalamu, upo mchakato uitwao ‘Neurogenesis’ ambao husaidia kulinda seli za ubongo zinazokufa kutokana na uzee. Kuna eneo kwenye ubongo linaloitwa ‘hippocampus’ ambalo ni eneo linalotengeneza kumbukumbu.

“Kazi kubwa inafanyika kwenye ubongo, wakati wa tendo la ndoa, kiasi kikubwa cha viamsha raha huanzia kwenye ubongo na kuleta taarifa kwenye maeneo mengine ya mwili.

Ndiyo maana watu wengi hupotea kiufahamu wakati wa kilele” anasema Dk Gosh, ambaye ni mtafiti.

Hata hivyo, wanaume ambao wanaendelea na tendo la ndoa mara kwa mara hadi wanapofikisha miaka 50 na zaidi, kwa maana ya kutoa mbegu za kiume mara kumi kwa mwezi, wapo katika hatari ndogo ya kupata saratani ya tezi dume.  Inaelezwa kuwa mbegu za kiume hazitakiwi kukaa mwilini kwa muda mrefu.Zinatakiwa zitolewe mara kwa mara ili kuzifanya seli mpya zizalishwe. Ni kama kusafisha mpira, inasaidia kusitisha ujenzi wa seli za zamani ambazo zaweza kuwa chanzo cha saratani.

Kwa wanawake, tendo la ndoa husaidia kuundwa kwa misuli ya nyonga ambapo misuli hiyo ikiwa imara huondoa hatari ya kushindwa kuzuia mkojo,(urine incotinence) jambo linaloathiri mwanamke mmoja kati ya wanne wenye umri wa miaka zaidi ya 50.

“ Wakati wa tendo la ndoa, kwa kawaida sakafu ya nyonga za mwanamke hubana na kuachia. Hii husababisha misuli hiyo kuwa imara’ anasema mtafiti huyo.



Hata hivyo,  utafiti wa Chuo Kikuu cha Nottingham nchini Uingereza  unaeleza kuwa,  wanaume wanaofanya tendo hilo na kumwaga mbegu mara 20 hadi 30 kwa mwezi, wapo katika hatari ya kupata saratani ya tezi dume kwa sababu ya umri wao .

Kuondoa maumivu ya kichwa


Utafiti mwingine umebaini kuwa, wanawake wenye umri mdogo hukumbwa na msongo wa mawazo iwapo hawatafanya tendo la ndoa kwa muda mrefu.

Wanawake hao, wanapofika kilele cha tendo hilo, damu hutembea kutoka kwenye ubongo,  jambo ambalo huondoa maumivu ya kichwa.

Dk Innocent Mosha, Mchunguzi wa magonjwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili anasema kuwa  inawezekana kuwa tendo la ndoa likasaidia kuondoa msongo wa mawazo iwapo mtu  hajalifanya kwa muda mrefu na yupo katika hali kubwa ya uhitaji.

“Kama mtu hajafanya tendo hilo muda mrefu na hivyo amelikamia, basi akilifanya litamwondolea msongo wa mawazo,” anasema

 Anasema mtu ambaye anahitaji kufanya tendo hilo na hajalipata, aghalabu huwa na msongo wa mawazo lakini kama huliwazi hawezi kuwa na msongo.

Kwenye utafiti huo, wanawake 83 wenye maradhi ya kichwa walipata nafuu kubwa baada ya kumaliza tendo la ndoa.

Ukaribu/ Upendo

Mwanasaikolojia, wa Chuo Kikuu cha Dodoma,  Modesta Kimonga anasema ni kweli kuwa tendo la ndoa linaleta faraja inayoondoa msongo wa mawazo.

 Anasema hali hiyo inatokana  na nadharia au mfumo wa uambatano katika saikolojia au ‘attachement theory’

“Hii ‘attachment theory’ ipo kwa watoto wanaponyonya maziwa ya mama zao, na kwa watu wazima ni kwenye tendo la ndoa ambalo linaleta faraja na ukaribu,” anasema.


Anaongeza:  “Faraja hupatikana baada ya wanandoa kutenda tendo hilo na huweza kuondoa kabisa mawazo kichwani au huzuni.”

Watafiti walibaini kuwa vichocheo vya ‘oxtocin’ vinavyotolewa wakati wa tendo hilo husaidia hisia za upendo na mshikamano kwenye uhusiano ya muda mrefu.

Lipo ongezeko kubwa la kemikali ya ‘oxtocin’ kwa wanawake na wanaume baada ya kumaliza tendo la ndoa ambalo husaidia kukuza uhusiano na ukaribu wao.

Wanaume kulala baada ya tendo la ndoa

Utafiti wa jarida la Sayansi ya Mishipa  ya Fahamu na Tabia uliochapishwa mwaka 2012 umebaini kuwa, dawa za usingizi hufanya kazi sawa na tendo la ndoa kwa wanaume.

 Eneo la mbele la ubongo ‘pre –frontal cortex’, ambalo linahusiana na  ufahamu, au umakini wa kiakili, huzima au kufungwa baada ya kumaliza tendo hilo.

 Kwa baadhi ya utafiti,  wanaume kumaliza tendo la ndoa,  ni sawa na kunywa dawa za usingizi za ‘diazepam’ zenye ukubwa wa miligramu mbili.

Pia, vichocheo vinavyotoka baada ya tendo hilo kama ‘melatonin,’ ‘oxytocin’ na ‘vasopresin’, zinamsababisha mwanaume apate usingizi mzito.


Chanzo:-Mwananchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad