Hii ndio Taswira ya kutelekezwa kwa Bwawa la Maji lililopo Mjini Sengerema maarufu kwa jina la Lambo la Mzungu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, February 10, 2014

Hii ndio Taswira ya kutelekezwa kwa Bwawa la Maji lililopo Mjini Sengerema maarufu kwa jina la Lambo la Mzungu.


Hili ndilo Bwawa lenyewe likiwa katika hali mbaya na kwa mazingira yalivyo sasa na halimashauri yetu ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kulitelekeza kwa kiasi hiki na kuzibwa na magugu maji kiasi cha kuhatarisha maisha ya wakazi wa mjini Sengerema,kwani kwa watoto ni rahisi sana kutumbukia kwani sehemu kubwa imezibwa na magugu maji ambapo unaweza kukanyaga ukijua ni mahali salama kwa kukanyaga kumbe kuna maji na kina kirefu.

Muonekano wa magugu maji yaliyojazana katika Bwawa hilo hali inayofanya uharibifu wa chanzo hicho muhimu cha maji mjini Sengerema.
Bwawa hilo lilikuwa ni tegemeo/likitumiwa na wakazi wengi wa mjini Sengerema kwa ajili ya matumizi ya maji majumbani na kwa wale wanafunzi wa miaka ya nyuma mtakumbuka umuhimu wa Bwawa hilo kwani ndilo lililokuwa likitumika siku za Jumamosi na Jumapili kwa ajili ya kufua na hata sasa linapojitokeza tatizo la ukosefu wa maji ya bomba toka ziwa victoria,wananchi wengi mjini Sengerema huenda kuchota maji katika Bwawa hilo.

Watu wazima na watoto wakipita juu ya tuta la Bwawa hilo,kingo hilo linaonekana kujaa majani hali inayohatarisha hata usalama wa wapitaji.

Muonekano wa Nyumba ya Mzee James Sosela ikiwa jirani kabisa na eneo lilipojengwa Dampo la takataka kama picha inavyoonekana.FU.

Shughuli za uvuvi wa samaki nazo zikiendelea katika Bwawa hilo lililoshindwa kuendelezwa na Serikali ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Vijana hawa wakiwa katika eneo lililo Kando na  Bwawa hilo wakijishughulisha na biashara ya kuotesha miti.

Ng'ombe wakiwa malishoni kando ya bwawa hilo lililopo mjini Sengerema…Picha Na:- eaglentertainment.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad