Matokeo Ligi Ulaya:-Manchester United na Juventus zalazimishwa sare huku FC Barcelona na Tottenham zikishinda michezo yao. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, February 10, 2014

Matokeo Ligi Ulaya:-Manchester United na Juventus zalazimishwa sare huku FC Barcelona na Tottenham zikishinda michezo yao.

David Moyes kichwa kinamuuma sana Man United pamoja na jitihada zote ikiwemo kumsajili Juan Mata kutoka Chelsea, lakini mambo bado magumu baada ya Februari 09,2014 Manchester United ikichomolewa dakika ya mwisho kabisa kwa bao Darren Bent na kulazimishwa sare ya 2-2 na Fulham,mchezo wa Ligi kuu soka Nchini Uingereza.


Matokeo haya yanaifanya United ya David Moyes ijiongezee pointi moja na kufikisha 41 baada ya kucheza mechi 25, ikiendelea kubaki nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi kuu.
Mabingwa watetezi wa Uingereza, Manchester United, licha ya kutawala Mechi yote, kukosa Nafasi nyingi mno na hata kuweza kutoka nyuma kwa Bao 1-0 na kumudu kuongoza kwa Bao 2-1 walikatwa maini katika Dakika ya 94 wakati Darren Bent aliposawazisha kwa Bao laini.

Ikiwa kinyume na Gemu ilivyokwenda, Fulham, ambao wako mkiani kwenye Ligi Kuu, walipata Bao la kuongoza laini wakati Difensi ya Man United ilipomegeka na kumruhusu Sidwell kukatiza kati na kufunga.

Kipindi cha Pili, Man United walifanya mabadiliko kadhaa kwa kuwaingiza kina Valencia, Januzaj na Chicharito na hii ilileta uhai na waliweza kufunga Bao 2 katika Sekunde 90.

Lakini kosa kosa zao za kufunga Bao la 3 kuliwagharimu kwani bila kutarajiwa Bent aliisawzishia Fulham kwenye Dakika za Majeruhi na kupata Sare ya Bao 2-2.

Mechi inayofuata kwa Man United ni hapo Jumatano(Februari 12,2014) huko Emirates watakapoivaa Arsenal ambayo (Februari 08,2014) ilikung’utwa Bao 5-1 na Liverpool huko Anfield.

Bao la Emmanuel Adebayor, la Dakika ya 65, limewapa ushindi wa Bao 1-0 Tottenham na kuishusha Everton toka Nafasi ya 5 na kukamata wao.
Position Team Played Goal Difference Points
1 Chelsea 25 27 56
2 Arsenal 25 22 55
3 Man City 25 41 54
4 Liverpool 25 33 50
5 Tottenham 25 0 47
6 Everton 25 11 45
7 Man Utd 25 10 41
8 Newcastle 25 -2 37
9 Southampton 25 7 36
10 Swansea 25 -3 27
11 Hull 25 -5 27
12 Aston Villa 25 -9 27
13 Stoke 25 -14 26
14 Crystal Palace 25 -16 26
15 West Ham 25 -7 25
16 Norwich 25 -18 25
17 Sunderland 25 -13 24
18 West Brom 25 -8 23
19 Cardiff 25 -25 21
20 Fulham 25 -31 20

Licha ya Juventus kutangulia kwa Bao 2 za mapema kupitia Carlos Tevez, Hellas Verona walirudisha Bao zote na kupata Sare ya Bao 2-2 walipocheza na Mabingwa hao wa Italy ambao pia ni Vinara wa Serie A huko Italy.

Baada Tevez kupiga Bao 2, Luca Toni aliifungia Hellas Verona Bao la kwanza na Muargetina Juanito Gomez kusawazisha katika Dakika ya 94.

Timu ya pili katika msimamo AS Roma nao walibanwa na kutoka Sare 0-0 Lazio.
Juventus sasa wamebaki kileleni wakiwa Pointi 9 mbele ya AS Roma na wako Pointi 13 mbele ya Timu ya Tatu Napoli ambao waliifunga AC Milan 3-1 hapo Jana Feb 08,2014 Jumamosi.

    Lazio 0 - 0 Roma
    Verona 2 - 2 Juventus
    Torino 1 - 2 Bologna
    Livorno 0 - 1 Genoa
    Parma 0 - 0 Catania
    Sampdoria 1 - 0 Cagliari
    Internazionale 1 - 0 Sassuolo

Position Team Played Goal Difference Points
1 Juventus 23 38 60
2 Roma 22 34 51
3 Napoli 23 20 47
4 Fiorentina 23 18 44
5 Internazionale 23 13 36
6 Verona 23 2 36
7 Parma 22 5 33
8 Torino 23 6 33
9 Lazio 23 0 32
10 Genoa 23 -4 30
11 Milan 23 1 29
12 Sampdoria 23 -5 28
13 Atalanta 23 -8 27
14 Udinese 23 -7 26
15 Cagliari 23 -11 24
16 Bologna 23 -17 21
17 Chievo 23 -16 18
18 Livorno 23 -19 17
19 Sassuolo 23 -26 17
20 Catania 23 -24 16

Nao Sevilla wakicheza nyumbani katika ligi kuu soka Hispania wamekubali kufungwa bao 4-1 na FC Barcelona kwa magoli ya Sánchez 34′ Messi 44′, 56′ Fábregas 88′ na kuwarejesha kileleni mwa msimamo wakiwa pointi 57 ila wanaubora mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa.

Position
Team
Played
Goal Difference
Points
1
Barcelona
23
46
57
2
Real Madrid
23
41
57
3
Atlético Madrid
23
40
57
4
Athletic Bilbao
22
14
43
5
Villarreal
23
17
40
6
Real Sociedad
23
8
37
7
Sevilla
23
1
31
8
Valencia CF
23
1
31
9
Espanyol
23
-3
29
10
Levante
23
-8
29
11
Celta de Vigo
22
-6
25
12
Elche
23
-12
25
13
Getafe
23
-14
25
14
Osasuna
23
-16
25
15
Almería
23
-17
25
16
Málaga
23
-10
24
17
Granada CF
23
-10
24
18
Real Valladolid
23
-13
21
19
Rayo Vallecano
23
-27
20
20
Real Betis
23
-32
14

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad