Tazama Ubovu wa barabara ulivyosababisha gari la Mkuu wa mkoa wa Njombe kukwama kwenye tope kijiji cha utweve makete. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 13, 2014

Tazama Ubovu wa barabara ulivyosababisha gari la Mkuu wa mkoa wa Njombe kukwama kwenye tope kijiji cha utweve makete.


Gari la mkuu wa mkoa wa Njombe, Kapteni mstaafu Aseri Msangi  likiwa limekwama kwenye tope kijiji cha utweve makete  wilayani Makete wakati akiwa ziarani kukagua maendeleo ya sekondari ya wasichana makete inayojengwa kijijini hapo.


Wanakijiji wakisukuma gari hilo, na huyu ni mwenyekiti wa kijiji cha Utweve akijitahidi kusukuma.

Hali tete hapa, gari hilo likiwa limenasa mtaroni kijiji cha utweve makete wilayani Makete wakati akiwa ziarani kukagua maendeleo ya sekondari ya wasichana makete inayojengwa kijijini hapo.

Gari la mkuu wa mkoa wa Njombe, Kapteni mstaafu Aseri Msangi likiwa limekwama kwa zaidi ya saa kadhaa katika kijiji cha Utweve wilayani Makete wakati akiwa ziarani kukagua maendeleo ya sekondari ya wasichana makete inayojengwa kijijini hapo.

Adha hiyo ilimkumba mkuu wa mkoa baada ya mvua kubwa kunyesha wakati akifanya mkutano na wananchi shuleni hapo mara baada ya kuikagua shule hiyo na kuridhishwa na jinsi ilivyojengwa.

Magari mengine yaliyokuwa yametangulia gari la mkuu wa mkoa yakipita eneo hilo lililokuwa na utelezi mwingi huku gari hilo la mkuu wa mkoa likikwama kutokana na utelezi huo.

Jitihada za kulinasua gari hilo zilifanywa na msafara mzima ulioambatana na mkuu wa mkoa pamoja na wananchi wa kijiji hicho ambapo zoezi hilo lilichukua zaidi ya saa moja kutokana na mvua kuzidi kunyesha zaidi.

Jitihada hizo zilizaa matunda na hatimaye gari hilo lilinasuliwa na mkuu wa mkoa kuendelea na safari yake, na hakuna madhara yoyote yaliyotokea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad