Tazama taswira ya Moto ulivyozuka katika stoo ya kuhifadhia vitu mbalimbali ya chuo cha taaluma ya Polisi mjini Moshi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 13, 2014

Tazama taswira ya Moto ulivyozuka katika stoo ya kuhifadhia vitu mbalimbali ya chuo cha taaluma ya Polisi mjini Moshi.

Wanafunzi wa chuo cha taaluma ya Polisi Moshi wakijaribu kuzima moto na kuokoa mali zilizokuwa zikiungua katika moja ya stoo ya kuhifadhia vitu mbalimbali zikiwemo nguo baada ya kuzuka kwa moto katika jengo hilo Jana Februari 12,2014. Hakuna mtu aliyeripotiwa kudhurika na Mkuu wa Chuo hicho Kamishana Msaidizi wa Polisi Matanga Mbushi ameahidi kutoa taarifa kamili baadaye.

Askari wanafunzi wakipambana na moto kwa kila jinsi wakijaribu kuzima moto na kuokoa mali zilizokuwa zikiungua katika moja ya stoo ya kuhifadhia vitu mbalimbali zikiwemo nguo baada ya kuzuka kwa moto katika jengo hilo Jana Februari 12,2014. Hakuna mtu aliyeripotiwa kudhurika na Mkuu wa Chuo hicho Kamishana Msaidizi wa Polisi Matanga Mbushi ameahidi kutoa taarifa kamili baadaye.
Picha juu na chini ni baadhi ya vitu vikiokolewa kutoka katika jengo lililowaka moto.
Sare za askari zikiwa zimeokolewa toka katika jengo hilo.
Moja ya kifaa kilichopo chuoni hapo ambacho pia kilikuwa kikitumika kwa shughuli za kuzima moto katika jengo hilo .Mkuu wa chuo hicho Matanga Mbushi amesema taarifa kamili ya moto huo itatolewa baadae.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akiwa na mkuu wa Chuo cha taaluma ya Polisi kamishana msaidizi wa polisi Matanga Mbushi wakishuhudia zoezi la uzimaji moto katika jengo hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad