Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Umma wa
CUF, Abdul Kambaya, amesema chama chake hakina mpango wa kusimamisha mgombea
katika jimbo hilo na kwamba hivi sasa wanaandaa mikutano ya kuimarisha chama
chao.
“Mpaka sasa CUF haina mpango wa kusimamisha mgombea
ubunge Kalenga… kwa sasa tunaandaa kikao cha Kamati Tendaji kitakachokaa kati
ya Februari 15 na 16 mwaka huu ili kujadili masuala mbalimbali,” alisema
Kambaya.
CHADEMA imepanga kumtangaza mgombea wa kiti hicho
wakati wowote baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kuketi mwishoni mwa wiki hii
kwa ajili ya kuteua jina la mgombea.
“Kwa sasa chama kinakusanya fomu za waliojitokeza
kugombea jimbo hilo… hadi sasa tunaendelea na zoezi hilo, mwamuzi wa mwisho ni
kamati kuu itakayoketi mwisho wa mwezi huu kwa ajili ya uteuzi wa jina hilo,”
alisema Ofisa Habari wa Chama hicho, Tumaini Makene.
Juzi CCM ilimtangaza Godfrey Mgimwa, mtoto wa
aliyekuwa mbunge wa Kalenga na Waziri wa Fedha na Uchumi, marehemu William Mgimwa, kugombea katika uchaguzi
mdogo, ambao kampeni zake zitaanza rasmi Februari 19, mwaka huu.
Mgimwa alichaguliwa kwa kura 348 za maoni za wajumbe
708 kati ya wajumbe halali 816 wa CCM katika mkutano mkuu wa jimbo hilo, na
aliibuka kidedea kati ya wagombea tisa waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment