Watu wanne
wapo katika hali mbaya na wengine saba wamejeruhiwa baada ya lori scania namba
T653 BFD (scania 380) kugongana uso kwa uso na baso dogo la abiria
Toyota Hiace T613 CPG iliyokuwa inatoka mbagala kwenda mkuranga.
Kwa mujibu
wa shuhuda ya ajali hiyo iliyotokea Mwandege, Dominic Kubhota, ameiambia blogu
hii , kwamba chanzo cha ajali hiyo ni ovateki isiyotumia akili ya lori
hilo .
Majeruhi hao wamefikishwa katika hospitali ya Mkuranga, lakini muda
mfupi baadaye walianza kukimbizwa kuleta Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Abiria
wawili waloikuwa mbele ya daladala walikatika miguu.
Majeruhi
wengine walioweza kuzungumza ni: Mustafa Mfungapoa wa mkuranga, Abdul Ally
wa Mwandege, Ramadhani Rajab, Theofrida Mwinuka ( alikuwa mbele amevunjika
miguu)Jamal mbaraka ( aliyekwanguka ngozi ya kichwa)Abraham Mohamed
Swalehe Salum.
Picha
na Lukaza Blog.
No comments:
Post a Comment